Imaam Ibn Al-Qayyim: Kuhusisha Siku Au Mahali Kwa ‘Ibaadah Bila Ya Dalili
Kuhusisha Siku Au Mahali Kwa ‘Ibaadah Bila Ya Dalili
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
Haikuamrishwa kuhusisha mahali palipoanza kuteremshwa Wahyi wala wakati kwa ‘ibaadah. Anayehusisha mahali au wakati kwa ‘ibaadah ni itikadi yake mwenyewe, na hivyo ni sawa na mfano Ahul-Kitaab ambao waliofanya wakati na matukio ya Al-Masiyh (Nabiy Iysaa) kuwa ni misimu ya ‘ibaadah kama siku ya kuzaliwa na siku ya kubatizwa na kadhalika.
[Zaad Al-Ma’aad fiy Had-yi Khayril-‘Ibaad (1/56-58)]