Vipai Vya Nyama (Meat Rolls)
Vipai Vya Nyama (Meat Rolls)
Vipimo
Siagi - Kikombe 1
Unga - Vikombe 2 (ufute, usijaze mlima)
Maji - Kiasi
Nyama ya kusaga - Kikombe 1
Pilipili manga ya unga - ½ kijiko cha chai
Kitunguu saumu(thomu) iliyosagwa - ½ kijiko cha chai
Tangawizi iliyosagwa - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna ya kutayarisha na kupika
Kutayarisha nyama:
- Changanya nyama, pilipili manga, thomu, tangawizi na chumvi ndani ya sufuria, ipike bila ya kutia mafuta wala maji huku unaikoroga koroga mpaka iwe kavu.
- Epua weka pembeni
- Changanya unga na siagi mpaka uchanganyike vizuri.
- Changanya na maji ili ushikane, lakini usiukande.
- Kata madonge na usukume kama unataka kufanya chapati, lakini usifanye mwembamba sana.
- Kata vipande virefu virefu. (rectengular)
- Weka nyama juu ya kila kipande, halafu kunja upande mmoja ufunike ile nyama, kisha kunja upande wa pili kufunika ile sehemu ya kwanza uliyoikunja.
- Chukua uma choma choma juu yake ili kuweka nakshi, pia utadidimiza ile sehemu ya mwisho iliyokunjwa kwa kuzuwia isifunuke wakati wa kuchoma.
- Fanya hivyo mpaka umalize zote.
- Chukua tray na kupaka siagi na uzipange humo.
- Washa overn na uzichome (Bake) 350 Deg C mpaka zibadilike rangi zikiwa tayari kuliwa.