116-Hiswnul-Muslim: Takbiyrah Atakapofika Katika Hajarul-Aswad
Hiswnul-Muslim .
116-Takbiyrah Atakapofika Katika Hajarul-Aswad
[234]
طَافَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِالْبَيْتِ عَلى بَعِيرٍ، كُلَّما أَتَى الرُّكْن أَشَارَ إِلَيْهِ بِشَيْءٍ عِنْدَهُ وَكَبَّرَ
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alitufu kuzunguka Al-Ka’bah juu ya ngamia. Kila alipofika katika rukn (Hajarul-Aswad) alikuwa anaashiria kwa kitu na kusema:
اللهُ أكْبَر
Allaahu Akbar
Allaah ni Mkubwa[1]
[1] Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/476), na ilokusudiwa ‘kitu’ ni fimbo yake. Angalia: Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/472).
Hajarul-Aswad: Jiwe jeusi lilioko pembe moja ya Al-Ka’bah