126-Hiswnul-Muslim: -Kinachopaswa Kusema Wakati Wa Mfazaiko
Hiswnul-Muslim
126-Kinachopaswa Kusema Wakati Wa Mfazaiko
لا إِلهَ إلاَّ اللهُ
Laa ilaaha illa-Allaah
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah[1]
[1]Hadiyth ya Zaynab bint Jahsh (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/181) [3346], Muslim (4/2208) [2880] na imekuja kikamilifu:
أَنّ النَّبِيَّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: ((لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ ، فُتِحَ الْيَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذِهِ)) وَحَلَّقَ بِإِصْبَعَيْهِ الإِبْهَامِ وَالَّتِي تَلِيهَا فَقُلْتُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنَهْلَكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ ؟ فَقَالَ: ((نَعَم ، إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ))
Nabiy alingia chumbani kwake akiwa katika hali ya kufazaika akasema:
لا إِلهَ إلاَّ اللهُ
((Laa ilaaha illa Allaah – hapana mwabudiwa wa hakiisipokuwa Allaah. Ole kwa Waarabu kutokana na shari iliyokaribia. Leo limefunguka shimo katika boma la kizuzi cha Ya-ajuwj na Ma-ajuwj kama hivi!)) Akafanya kiduara kwa kufunga kidole chake cha gumba na cha shahada. Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hivi tutaangamia na hali tumo watu wema?”Akasema: ((Ndio pindi maovu yakizidi)).