Choroko Za Kupaaza Za Nazi

Choroko Za Kupaaza Za Nazi

Vipimo

Choroko za kupaaza  - 1 kikombe kikubwa (mug) 

Kitunguu maji  - 1 kimoja

Binzari ya manjano ya unga -   1/2 kijiko cha chai 

Kitungu saumu(thomu/galic) -  1 kijiko cha chai 

Nyanya -  1 moja

Pilipili nzima -   1-2 

Chumvi -  kiasi 

Nazi -  1 kikopo (400-500 mls)  

Namna Ya Kutayarisha

 1. Osha choroko zako vizuri na zichemshe kwa maji ya kiasi tu hadi ziwive na zisivurugike.
 2. Katakata kitunguu maji vipande vidogodogo.
 3. Imenye nyanya maganda halafu iponde.

Namna Ya Kupika 

 1. Weka sufuria jikoni na moto wa kiasi tia mafuta kidogo.(kijiko kikubwa cha kulia)
 2. Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi kidogo
 3. Tia binzari ya manjano kaangia kidogo
 4. Kisha tia vitunguu thaumu kaanga kidogo.
 5. Halafu mimina nyanya iliyosagwa na chumvi kiasi.
 6. Acha ikaangike huku ukikoroga.(kama dakika 5-10 hivi)
 7. Kisha mimina choroko zilizoshemshwa changanya acha maji yakauke kiasi
 8. Mimina nazi na onja chumvi kama imekolea punguza moto acha nazi ichemkie, kiasi cha kuacha urojo wa kutosha.
 9. Mwisho katia pilipili ziwivie kiasi.

 

Zikisha kuwa tayari mimina kwenye bakuli lako tayari kwa kuliwa na chapati , wali  hata pita bread (mkate)

Share