012-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ruhusa Kuwalaani Watu wa Maasi Bila Kuwataja Majina

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب جواز لعن أصحاب المعاصي غير المعينين

012-Mlango Wa Ruhusa Kuwalaani Watu wa Maasi Bila Kuwataja Majina

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾

Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu. [Huwd: 18]

فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾

Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu! [Al-A'raaf: 44]

 

وَثَبَتَ فِي الصَّحِيحِ أَنَّ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( لَعنَ اللهُ الوَاصِلَةَ وَالمُسْتَوْصِلَةَ )) وَأنَّهُ قَالَ : (( لَعَنَ اللهُ آكِلَ الرِّبَا )) وأنَّهُ لَعَنَ المُصَوِّرِينَ ، وأنَّهُ قَالَ : (( لَعَنَ اللهُ مَنْ غيَّرَ مَنَارَ الأَرْضِ )) أيْ حُدُودَهَا ، وأنَّهُ قَالَ : (( لَعَنَ اللهُ السَّارِقَ يَسْرِقُ البَيْضَةَ ))  ، وأنَّهُ قَالَ : (( لَعَنَ اللهُ مَنْ لَعَنَ وَالِدَيهِ )) وَ(( لَعَنَ اللهُ من ذَبَحَ لِغَيْرِ اللهِ )) ، وَأنَّه قَالَ : (( مَنْ أَحْدَثَ فِيهَا حَدَثاً أَوْ آوَى مُحْدِثاً فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللهِ وَالمَلاَئِكَة والنَّاسِ أجْمَعينَ )) ، وأنَّه قَالَ : (( اللَّهُمَّ الْعَنْ رِعْلاً ، وَذَكْوَانَ، وعُصَيَّةَ : عَصَوُا اللهَ وَرَسُولَهُ )) وهذِهِ ثَلاَثُ قَبَائِلَ مِنَ العَرَبِ . وأنَّه قَالَ : (( لَعَنَ اللهُ اليَهُودَ اتَّخَذُوا قُبُورَ أنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ )) وأنهُ (( لَعَنَ المُتَشَبِّهِينَ مِنَ الرِّجَالِ بالنِّساءِ والمُتَشَبِّهاتِ مِنَ النِّسَاءِ بالرِّجالِ ))  .

وَجَميعُ هذِهِ الألفاظِ في الصحيح ؛ بعضُها في صَحيحَيّ البُخاري ومسلمٍ ، وبعضها في أحَدِهِمَا ، وإنما قصدت الاختِصَارَ بالإشارةِ إِلَيهمَا ، وسأذكر معظمها في أبوابها من هَذَا الكتاب ، إن شاء الله تَعَالَى .

 

Imethubutu katika Hadiyth Swahiyh kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake kwa nywele nyengine na mwenye kutaka kufanywa hivyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na kuwa pia amesema: "Allaah Amemlaani mwenye kula riba." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na kuwa yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amemlaani anayechora picha." [Al-Bukhaariy].

 

Na kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Amemlaani mwenye kubadilisha au kufuta mipaka ya ardhi." [Muslim]. Na kuwa amesema: "Allaah Amemlaani mwizi mwenye kuiba hata yai." [Al-Bukhaary na Muslim]. Na kuwa amesema: "Allaah Anamlaani mwenye kuwalaani wazazi wake." [Muslim]. Na pia: "Allaah Amemlaani mwenye kuchinja kwa asiyekuwa Allaah." [Muslim]. Na kuwa amesema: "Mwenye kuzua jambo baya ndani yake (Katika mji wa Madiynah) uzushi au kuanzisha jambo (Linalokwenda kinyume na sheria), juu yake iwe laana ya Allaah, Malaaikah Zake na watu wote kwa jumla." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na pia amesema: "Ee Allaah! Walaani Ri'lan, na Dhakwaan, na 'Uswayyah, kwani wamemuasi Allaah na Rasuli Wake." [Muslim]. Na haya ni makabila matatu ya Kiarabu. Na pia amesema: "Allaah Awalaani Mayahudi, kwani wamefanya makaburi ya Manabiy wao kuwa ni Msikiti." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na amesema: "Wamelaaniwa wanaume wenye kujifananisha na wanawake, na wanawake wenye kujifananisha na wanaume." [Al-Bukhaary].

 

Na lafdhi zote zipo katika Swahiyh, baadhi yake zipo katika Swahiyh ya Al-Bukhaary na Muslim, na baadhi yake katika moja wapo ya Swahiyh hizo mbili. Na hakika nilikusudia kuzileta kwa muhtasari kwa kuziashiria. Na nitazitaja nyingi miongoni mwazo katika milango mingine ya kitabu hichi, Anapo penda Allaah Ta'aalaa.

 

Share