013-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumtusi Muislamu Bila ya Haki

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم سب المسلم بغير حق

013-Mlango Wa Kukatazwa Kumtusi Muislamu Bila ya Haki

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]

 

Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( سِبَابُ المُسْلِمِ فُسُوقٌ ، وَقِتالُهُ كُفْرٌ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kumtukana Muislamu ni ufasiki na kumwua ni ukafiri." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي ذرٍ رضي اللهُ عنه : أنهُ سَمِعَ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقول : (( لاَ يَرْمِي رَجُلٌ رَجُلاً بِالفِسْقِ أَوِ الكُفْرِ ، إِلاَّ ارْتَدَّتْ عَلَيْهِ ، إنْ لَمْ يَكُنْ صَاحِبُهُ كذَلِكَ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mtu hamwiti mtu mwengine kuwa ni fasiki au kafiri isipokuwa hurudi kwake sifa hiyo ikiwa mwenye kuitwa hana jambo hilo." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( المُتَسَابَّانِ مَا قَالاَ فَعَلَى البَادِي منهُما حَتَّى يَعْتَدِي المَظْلُومُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wanapo tukanana watu wawili, yule aliyeanza ndiye mwenye kulaumiwa mpaka atakapovuka mipaka aliye dhulumiwa." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه، قَالَ : أُتِيَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، بِرَجُلٍ قَدْ شرِبَ قَالَ : (( اضربوهُ )) قَالَ أَبُو هريرةَ : فَمِنَّا الضارِبُ بيَدِهِ ، والضَّارِبُ بِنَعْلِهِ ، والضَّارِبُ بِثَوْبِهِ . فَلَمَّا انْصَرَفَ ، قَالَ بَعْضُ القَوْمِ : أخْزَاكَ اللهُ ! قَالَ : (( لا تَقُولُوا هَذَا ، لا تُعِينُوا عَلَيْهِ الشَّيْطَان )) . رواه البخاري .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliletwa mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amekunywa pombe, akasema: "Mpigeni." Akasema Abu Huraiyrah: "Kuna miongoni mwetu waliompiga kwa mikono, na wengine kwa viatu na wengine kwa nguo zao." Alipoondoka yule mtu, baadhi ya watu walianza kusema: "Allaah akupe hizaya." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Musiseme hivyo, musimsaidie shetani juu yake." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقول : (( مَنْ قَذَفَ مَمْلُوكَهُ بِالزِّنَى يُقَامُ عَلَيْهِ الحَدُّ يَومَ القِيَامَةِ ، إِلاَّ أَنْ يَكُونَ كما قَالَ )) . متفق عَلَيْهِ .

Amsema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kumtuhumu mtumwa wake kuwa amezini atasimamishwa adhabu Siku ya Qiyaamah isipokuwa iwe ni kama alivyosema (iwe ni kweli)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share