Maulidi: Sababu 35 Muislam Asisherehekee Maulidi

 

Sababu 35 Muislam Asisherehekee Maulidi

 

 Alhidaaya.com

 

 

AlhamduliLLaah, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Zifuatazo ni baadhi ya hoja za wazi kutoka katika Qur-aan na Sunnah zinazopinga Maulidi, tukitumai kuwa zitamtosheleza Muislamu aikinaishe nafsi yake kuwa Maulidi ni jambo la uzushi katika Dini.

 

Sababu Ya Kwanza:

 

Kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

Kwa sababu ya kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kumfuata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tokea kuzaliwa kwake hadi kufariki kwake hakusherehekea siku yake ya kuzaliwa wala Maswahaba zake hawakumsherehekea. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-'Imraan: 31] 

 

 

Sababu Ya Pili:

 

Kufuata amri ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kushikamana na Sunnah Zake na Sunnah za Makhalifa wake kwa vile amesema:

 ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا. فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ)) رواه أبو داود، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح

((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrishen) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu.  Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuwd, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]   

 

 

Sababu Ya Tatu: 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatuamrisha tufuate aliyotuletea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tujiepushe na yale aliyotukataza. Anasema:  

  وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ

Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni.  [Al-Hashr: 7]

 

 

Sababu Ya Nne:

 

Kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ

Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli.  [At-Twaghaabun: 12]

Na kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kumtii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao [An-Nisaa: 80]

 

 

Sababu Ya Tano:

 

Kutokufuata amri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwenda kinyume naye na ni sababuu ya kupata adhabu kali. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.  [An-Nuwr: 63]

 

 

Sababu Ya Sita: 

Kumpinga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni sababu ya kuingizwa motoni. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾

Na atakayempinga Rasuli baada ya kuwa imeshambainikia Uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini; Tutamgeuza alikogeukia (mwenyewe upotofuni) na Tutamuingiza Jahannam. Na uovu ulioje mahali pa kuishia.    [An-Nisaa: 115]

 

 

Sababu Ya Saba:

 

Kukhofia upotofu ambao unampeleka mtu motoni.

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitanguliza khutba zake kwa kutoa maonyo hayo:

((إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه 

((Maneno bora ni kitabu cha Allaah (Qur-aan) na Uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika Dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake] 

 

 

Sababu Ya Nane:  

 

Kuhofia kuwa miongoni mwa kundi litakaloingia motoni.

 

Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((افترقت اليهود على إحدى وسبعين فرقة، وافترقت النصارى على اثنتين وسبعين فرقة، وستفترق هذه الأمة على ثلاث وسبعين فرقة كلها في النار إلا واحدة)) فقال الصحابة: من هي يا رسول الله؟ قال: ((من كان على مثل ما أنا عليه وأصحابي)) الترمذي والحاكم

((Waligawanyika Mayahudi katika makundi sabini na moja, na waligawanyika Manaswara katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika Umma wangu katika makundi sabini na tatu, yote yataingia motoni ila moja!)) Maswahaba wakasema: 'Ni kundi lipi hilo Ee Rasuli wa Allaah?  Akajibu: ((Ni lile ambalo litakuwa katika mwenendo wangu hii leo na Maswahaba zangu)) [Imepokewa na Maimaam At-Tirmidhiy na Al-Haakim]

 

 

Sababu Ya Tisa:

 

Kuitikia wasiya wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ili kubakia katika njia iliyonyooka.  Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

  وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

 “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.”   [Al-An'aam: 153]

 

 

Sababu Ya Kumi:

 

Vitendo visivyokuwa vya Sunnah havipokelewi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 ((من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]

Hivyo mtu atapoteza muda wake, labda na gharama ya kutekeleza bid'ah hii na kumbe amali hii haina thamani yoyote mbele ya Allaah.

 

 

Sababu Ya Kumi Na Moja:

 

Mwezi huu wa Rabiy'ul Awwal ni mwezi aliofariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sasa vipi Muislamu asherehekee kifo chake?

 

Wanachuoni wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah wameafikiana kuwa tarehe 12 Rabiy‘ul-Awwal ni siku aliyofariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).  Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema:

 

لمَّا كانَ اليومُ الَّذي دخلَ فيهِ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ المدينةَ أضاءَ منْها كلُّ شيءٍ، فلمَّا كانَ اليومُ الَّذي ماتَ فيهِ أظلمَ منْها كلُّ شيءٍ، ونفَضنا عن رسولِ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ الأيدي وإنَّا لفي دفنِهِ حتَّى أنْكَرنا قلوبَنا

Siku ambayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Madiynah kila kitu kiliingia mwanga. Na siku aliyofariki kila kitu kiliingia kiza, kisha tulipomzika tukafuta vumbi mikononi mwetu, tukahisi nyoyo zetu zimebadilika. [Swahiyh Ibn Maajah (1332), Swahiyh At-Tirmidhiy (3618)]  

 

 

Sababu Ya Kumi Na Mbili:

 

Maulidi yamezushwa karne ya nne (miaka mia nne) baada ya kufariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na yamezushwa na wapotofu:

Walioanzisha Maulidi ni viongozi wa Faatwimiyyuwn huko Misr (hawa walikuwa ni Rawaafidhw (Mashia) katika dhehebu la Ismailiyah [Makoja] walianza kusherehekea Maulidi ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu), na Maulidi ya Hasan na Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa), na Maulidi ya Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa), na Maulidi ya kiongozi wao aliye hai kwa wakati ule. Basi kwanini Muislamu awafuate wao na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametudhihirishia kuwa watu bora kabisa wa kuwafuata ni wa karne tatu pekee aliposema:

 

((خير القرون قرني ثم الذين يلونهم ثم الذين يلونهم)) متفق عليه 

((Karne zilizo bora kabisa ni karne yangu, kisha inayofuatia kisha inayofuatiya)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Sababu Ya Kumi Na Tatu:

 

Baadhi ya maneno katika Maulidi yana kufru kwa kuwa yanampandisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) cheo sawa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na hali yeye mwenyewe ametuonya:

 

 ((لا تطروني كما أطرت النصارى المسيح ابن مريم، إنما أنا عبد، فقولوا: عبد الله ورسوله)) متفق عليه

((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Sababu Ya Kumi Na Nne: 

 

Wanaosoma Maulidi, pale wanapoinuka baada ya beti fulani za Maulidi zinazotajwa mazazi yake, wanaamini kwamba roho yake inahudhuria wakati huo!

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe alikuwa hapendi kuinukiwa alipokuwa hai, basi vipi afanyiwe jambo asilolipenda baada ya kufariki kwake?   

عَنْ أَنَسٍ قَالَ‏:‏ مَا كَانَ شَخْصٌ أَحَبَّ إِلَيْهِمْ رُؤْيَةً مِنَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم، وَكَانُوا إِذَا رَأَوْهُ لَمْ يَقُومُوا إِلَيْهِ، لِمَا يَعْلَمُونَ مِنْ كَرَاهِيَتِهِ لِذَلِكَ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba hakuweko mtu waliyependa kumuona zaidi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini walikuwa wanapomuona hawakuwa wakimuinukia kwa kuwa walijua kuwa alikuwa anachukia hivyo. [Swahiyh Adab Al-Mufrad (724) na akaitaja tena Al-Albaaniy Rahimahu Allaah katika darsa ya “Karaahiyyah Ar-Rasuwl Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam liqiyaam lahu”]

 

 

Sababu Ya Kumi Na Tano:

 

Katika Maulidi kuna maasi ya kuchanganyika wanawake na wanaume:

Na wengine huimba qaswiydah zao huku wakichezesha miili kama kwamba ni dansi fulani. Imefika hadi Maulidi kuitwa ‘disco Maulidi’

 

 

Sababu Ya Kumi Na Sita: 

 

Maulidi ni kuwaigiza Manaswara

 

Manaswara wanasherehekea siku ya kuzaliwa Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam). Waislamu nao wakaiga na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuwaigiza makafiri aliposema:

 

 ((خالفوا المشركين، أحفوا الشوارب، وأوفوا اللحى)) البخاري ومسلم

((Kuweni kinyume na Washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na pia akasema:

 ((من تشبه بقوم فهو منهم)) أحمد وأبو داود

Anayejishabihisha na watu basi naye ni miongoni mwao)) [Ahmad, Abu Daawuwd]

 

 

Sababu Ya Kumi Na Saba:  

 

Dini imekamilika hakuna tena haja ya kuleta mambo mapya:

Kuzusha mambo mapya ya dini ni kama   kudai kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukamilisha ujumbe aliotumwa nao na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amethibitisha kuwa Dini Yake Ameikamilisha:

 

عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ إِلَى عُمَرَ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، آيَةٌ فِي كِتَابِكُمْ تَقْرَؤُونَهَا، لَوْ عَلَيْنَا نَزَلَتْ مَعْشَرَ الْيَهُودِ، لَاتَّخَذْنَا ذَلِكَ الْيَوْمَ عِيدًا. قَالَ: وَأَيُّ آيَةٍ؟ قَالَ: ((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الْإِسْلَامَ دِينًا)) فَقَالَ عُمَرُ: إِنِّي لَأَعْلَمُ الْيَوْمَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، وَالْمَكَانَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، نَزَلَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ، بِعَرَفَاتٍ، فِي يَوْمِ جُمُعَةٍ.

 Twaariq bin Shihaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikuja Myahudi mmoja kwa ‘Umar akasema: Ee Amiri wa Waumini! Aayah katika Kitabu chenu mnaisoma, kama ingeteremkwa kwetu hadhara ya Mayahudi, basi bila shaka tungeifanya siku hiyo kuwa ni siku ya kusherehekea! Akasema (‘Umar): Aayah ipi? Akasema: ((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu na Nimekutimzieni Neema Zangu kwenu na Nimekuridhieni Uislamu kuwa ni Diyn yenu)) [Al-Maaidah (5: 3] ‘Umar akasema: Hakika naijua siku gani imeteremka Aayah hii, na sehemuu iliyoteremkia, imeteremka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ‘Arafah, siku ya Ijumaa.  [Muslim]

 

Sasa vipi watu walete mafundisho mapya ya Dini? Anauliza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ

Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea idhini?  [Ash-Shuwraa: 21]

 

 

Sababu Ya Kumi Na Nane:

 

Kutokusherehekea Maulidi ni kudhihirisha iymaan ya Muislamu kwa kupenda kufuata yale aliyokuja nayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pekee:  

 

عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ "الْحُجَّةِ" بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.   

Kutoka kwa Abuu Muhammad ‘Abdullah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hatokuwa kaamini (kikwelikweli) mmoja wenu mpaka mapenzi yake yatakapomili (yatakapotii au kuwafikiana) kwenye yale niliyoyaleta)) (mafundisho) [Hadiyth Hasan iliyotoka katika kitabu “Al-Hujjah” ikiwa na mtiriko mzuri wa mapokezi].

 

 

Sababu Ya Kumi Na Tisa:

 

Kutokusherehekea ni kuacha mambo yenye shaka na kubakia katika yasiyo na shaka:

 

 عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ)) رَوَاهُ التِّرْمذِيُّ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Aliy Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kipenzi chake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: "Nilihifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maneno haya: ((Acha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka)). [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy akisema kuwa ni Hadiyth Hasan na Swahiyh].

 

 

Sababu Ya Ishirini:

 

Wanavyuoni wote wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah (Salafiyyah) wamepinga Maulidi.

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Moja: 

 

Watu wa Maulidi, wanadai kuwa kuna watu wasio Waislamu wamesilimu wengi kwa sababu ya Maulidi!!

 

Ikiwa kweli wapo waliosilimu kwa sababu ya Maulidi, basi ni kutokana na kuvutika kwao na zile shamrashamra zilizomo katika Maulidi, na hajasilimu kwa sababu ya kuupenda Uislamu na kuufahamu. Na aghlabu mtu kama huyo, atabakia kuwa ni mwenye kupenda zile shamrashamra tu na siku akibainikiwa kuwa hayo hayapo katika dini, basi hatokuwa na haja na Uislamu huo tena wa Maulidi. Ni sawa na wale wanaosilimu kwa kupendana na wanawake wa Kiislamu, na siku wakikorofishana au kuachana, anaacha na Uislamu.

Kadhaalika, ikiwa wako wanaosilimu kwa sababu ya Maulidi, basi watakuwa ni wale waliotoka katika zile dini za kuimba na kudansi makanisani au zile dini za kimila za kuimba na kucheza katika kila tukio; katika ndoa, katika msiba, katika matambiko, katika maombi, katika vita n.k.

 

Kwa hiyo, hoja hiyo ya kizembe, ni hoja ambayo inazidi kumkinaisha Muislamu kukirihishwa na uzushi huu wa Maulidi na kukaa nao mbali.

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Mbili: 

 

Wasiosherehekea Maulidi na wanaosherehekea wako baina ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾

Na hakika ima sisi au nyinyi, bila shaka tuko juu ya Uongofu au katika upotofu bayana.” [Sabaa: 24]

 

Kwa sababu haiwezekani ikawa wenye kuzusha katika Dini wako sawa na wanaofuata yaliyokuja kutoka Kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wema waliotangulia na kushikamana na Sunnah zake.

 

Kwa hiyo nani aliyesalimika? Ambaye anafuata Sunnah na maamrisho ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au anayefuata Mashia wapotofu walioanzisha Maulidi baada ya karne tatu bora?

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Tatu:

 

Kutukuza siku aliyozaliwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumfuata yeye mwenyewe alivyokuwa akifanya kwa kufunga Swawm siku ya Jumatatu (na Alkhamiys) kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo, na si kwa kufanya jambo asilolifanya kamwe!

 

عنْ أَبِي قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الِاثْنَيْنِ فَقَالَ: ((فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ)).

Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Swawm ya Jumatatu akasema: “Nimezaliwa siku hiyo na siku hiyo nimeteremshiwa (Qur-aan).” [Muslim]

 

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Nne:

 

Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kunahitajia kufuata vile alivyotuamrisha tumswalie na si kwa mitindo mingine au kwa muundo mwengine. Sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alipotuamrisha tumswalie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qur-aan, Maswahaba walitaka kujua jinsi ya kumswalia na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawafundisha kuwa ni kumswalia kama tunavyomswalia katika Swalaah na si kusherehekea mazazi yake. Dalili ni Hadiyth Swahiyh:

عنْ أبي مسْعُود الْبدْريِّ، رضي اللَّه عنْهُ، قالَ: أَتاناَ رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، وَنَحْنُ في مَجْلِس سعد بنِ عُبَادَةَ رضي اللَّه عنهُ، فقالَ لهُ بَشِيرُ بْنُ سعدٍ: أمرَنَا اللَّه أنْ نُصلِّي علَيْكَ يا رسولَ اللَّهِ، فَكَيْفَ نُصَّلي علَيكَ؟ فَسكَتَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، حتى تَمنَّيْنَا أنَّه لمْ يَسْأَلْهُ، ثمَّ قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ((قولُوا: اللَّهمَّ صلِّ عَلى مُحَمَّدٍ، وَعَلى آلِ مُحمَّدٍ، كما صليْتَ على آل إبْراهِيم، وَبارِكْ عَلى مُحَمَّد، وعَلى آلِ مُحمَّد، كما بَاركْتَ عَلى آل إبْراهِيم، إنكَ حمِيدٌ مجِيدٌ، والسلام كما قد عَلِمتم)) رواهُ مسلمٌ

Imepokelewa kwa Abuu Mas'uwd Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alitujia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na sisi tulikuwa katika majlisi ya Sa'ad bin 'Ubaadah (Radhwiya Allaahu 'anhu). Bashiyr bin Sa'ad akamwambia: Allaah Ametuamrisha tukuswalie ee Rasuli wa Allaah. Je, vipi tukuswalie? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza mpaka tukatamani kwamba asingelimuuliza. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Semeni: Allaahumma Swalli 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kamaa Swallayta 'alaa aali Ibraahiym, wa Baarik 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kama Baarakta 'alaa aali Ibraahiym Innaka Hamiydun-Majiyd. Na salaam kama mlivyofundishwa)) [Muslim]

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Tano:

 

Kumtambulisha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumtukuza na kumsifu ili makafiri wamtambue si kwa kufanya bid’ah ya Maulidi, bali kwa kuwadhihirishia tabia za Uislamu alizokuja nazo yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akatufundisha yeye ili makafiri wavutike nazo. 

 

Kadhaalika, kuwafundisha makafiri Siyrah yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuisambaza kwa kila njia kila siku na si kwa siku moja tu katika mwaka kwa kusoma Maulidi. Basi pima na jiulize! Je, njia ipi ni ya wingi zaidi kumtambulisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa makafiri ili waingie Uislamuni? Je ni mara moja tu kwa mwaka au kila siku? Kwa sababu wazushi husema: “Maulidi imewaingiza watu katika Uislamu!”

 

Na katika Siyrah Sahihi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kunapatikana miujiza yake yote, na sifa zake zote, tabia zake zote, na utukufu wake wote ambao unawatosheleza Makafiri kumkubali ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anataka kuwaongoa. Kama vile tunavyoona Makafiri wengi wanavyomkubali pindi wanapomjua na kumsoma na wakaingia Uislamu kwa wingi mno kama tunavyoshudia zama hizi.

 

Na sababu ya kuingia Usilamu watu ni kutokana na miujiza inayopatikana katika Qur-aan na mengineyo katika Siyrah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na hata hao makafiri wanaoingia Uislamu, wengi wao hufuata ya sahihi kwa kushikamana na Sunnah na wanajiepusha na bid’ah si kama wale Waislamu waliozaliwa ndani ya Dini lakini wakaiharibu kwa bid’ah zao! 

 

Juu ya hivyo Dini ya Kiislamu haihitaji uzushi wa Maulidi wala uzushi wowote ule ili Dini isambae kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi Mwenyewe kuidhihirisha juu ya dini nyinginezo kwa mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na yaliyo ya haki si ya uzushi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٢٨﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fat-h:  28. Aayah hii imekariri kwa kufanana kwake katika Suwrah At-Tawbah: 33, Asw-Swaff: 9]

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Sita:

 

'Ibaadah zimejengeka kwa tawqiyfiy (kama ilivyopokelewa kutoka katika Qur-aan na Sunnah) na si kutokana na rai. Ingekuwa siku ya kuzaliwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo linalopaswa, basi ingelipatakana dalili yake katika Dini, kama ilivyopatikana dalili kuhusu 'ibaadah za masiku mengineyo mfano 'ibaadah katika siku ya Ijumaa, 'Arafah, 'Aashuraa, Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja), masiku kumi ya Dhul-Hijjah, usiku wa Laylatul-Qadr n.k.  Kwa hiyo hata 'ibaadah ionekane nzuri vipi madamu hakuna burhaan (dalili wazi) kutoka katika Qur-aan na Sunnah basi halikubaliki. (Rejea sababu ya kumi upate dalili ya Hadiyth). Na ikiwa hakuna dalili ya wazi kuhusu kusherehekea Maulidi basi tanabahi kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾

Na wasipokuitikia basi jua kwamba hakika wanafuata hawaa zao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata hawaa zake bila ya Mwongozo kutoka kwa Allaah? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu. [Al-Qaswasw: 50]

 

Na pia tanabahi kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, Tukujulisheni wenye kukhasirika mno kwa ‘amali?”

الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾

Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia, na huku wao wakidhani kwamba wanapata mazuri kwa matendo yao. [Al-Kahf: 103-104]

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Saba:

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hakuadhimisha mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qur-aan bali kaadhimisha kupewa kwake Unabiy kama Anavyosema:

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunna); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Aal-‘Imraan: 163]

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Nane:

 

Kuzusha bid’ah ya Maulidi, kunafungua milango ya bid’ah nyinginezo humo katika siku hiyo ya sherehe, kama vile kutenga siku hiyo kusimulia siyrah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kuimba qaswiydah, kudansi wanapoimba, michanganyiko ya wake kwa waume, kupiga madufu Misikitini n.k.

 

Kadhaalika bid'ah zingine zikazuka kwa mlango huo huo wa kujifanya kuonesha mapenzi na kutukuza, kama bid’ah za kusherehekea Israa wal Mi’raaj, mwaka mpya wa hijrah, nisfu Sha'baan n.k.

 

 

Sababu Ya Ishirini Na Tisa:

 

Kubaki katika Swiraatw Al-Mustqiym na katika mipaka ya shariy’ah za Dini ni kubaki katika Sunnah bila ya kuongeza mambo katika Dini wala kuzusha. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametubainishia maana yake:

 

Imepokelwa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akachora mstari mbele yake, akachora mistari miwili kuliani, na misitari miwili kushotoni kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasema: “Hii njia ya Allaah” Kisha akasoma: “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni, na wala msifuate njia (nyinginezo) zitakufarikisheni na njia Yake.” [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah] 

 

 

Sababu Ya Thelathini:

 

Maswahaba walikhofia mno kuzusha katika Dini hata kama ni ‘ibaadah adhimu za kumdhukuru Allaah. Dalili ni Hadiyth:

 

عن عمرو بن سلمة (رضي الله عنه): كُنَّا نَجْلِسُ عَلَى بَابِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَبْلَ صَلاَةِ الْغَدَاةِ فَإِذَا خَرَجَ مَشَيْنَا مَعَهُ إِلَى الْمَسْجِدِ، فَجَاءَنَا أَبُو مُوسَى الأَشْعَرِيُّ فَقَالَ: َخَرَجَ إِلَيْكُمْ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ بَعْدُ؟ قُلْنَا لاَ: فَجَلَسَ مَعَنَا حَتَّى خَرَجَ، فَلَمَّا خَرَجَ قُمْنَا إِلَيْهِ جَمِيعًا فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ إِنِّي رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ آنِفًا أَمْرًا أَنْكَرْتُهُ وَلَمْ أَرَ وَالْحَمْدُلِلَّهِ إلاَّ خَيْرًا. قَالَ: فَمَا هُوَ؟ فَقَالَ: إِنْ عِشْتَ فَسَتَرَاهُ. قَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ قَوْمًا حِلَقًا جُلُوسًا يَنْتَظِرُونَ الصَّلاَةَ، فِي كُلِّ حَلْقَةٍ رَجُلٌ وَفِي أَيْدِيهِمْ حَصًى. فَيَقُولُ، كَبِّرُوا مِائَةً، فَيُكَبِّرُونَ مِائَةً، فَيَقُولُ هَلِّلُوا مِائَةً، فَيُهَلِّلُونَ مِائَةً، وَيَقُولُ سَبِّحُوا مِائَةً، فَيُسَبِّحُونَ مِائَةً، قَالَ: فَمَاذَا قُلْتَ لَهُمْ؟ قَالَ: مَا قُلْتُ لَهُمْ شَيْئًا انْتِظَارَ رَأْيِكَ وَانْتِظَارَ أَمْرِكَ. قَالَ أَفَلاَ أَمَرْتَهُمْ أَنْ يَعُدُّوا سَيِّئَاتِهِمْ وَضَمِنْتَ لَهُمْ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِهِمْ؟  ثُمَّ مَضَى وَمَضَيْنَا مَعَهُ حَتَّى أَتَى حَلْقَةً مِنْ تِلْكَ الْحِلَقِ فَوَقَفَ عَلَيْهِمْ فَقَالَ. مَا هَذَا الَّذِي أَرَاكُمْ تَصْنَعُونَ؟ قَالُوا: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ حَصًى نَعُدُّ بِهِا لتَّكْبِيرَ وَالتَّهْلِيلَ وَالتَّسْبِيحَ. قَالَ: فَعُدُّوا سَيِّئَاتِكُمْ فَأَنَا ضَامِنٌ أَنْ لاَ يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِكُمْ شَيْءٌ وَيْحَكُمْ يَا أُمَّةَ مُحَمَّدٍ، مَا أَسْرَعَ هَلَكَتَكُمْ هَؤُلاَءِ صَحَابَةُ نَبِيِّكُمْ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مُتَوَافِرُونَ وَهَذِهِ ثِيَابُهُ لَمْ تَبْلَ وَآنِيَتُهُ لَمْ تُكْسَرْ. وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّكُمْ لَعَلَى مِلَّةٍ هِيَ أَهْدَى مِنْ مِلَّةِ مُحَمَّدٍ أَوْ مُفْتَتِحُو بَابِ ضَلاَلَةٍ. قَالُوا: وَاللَّهِ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ مَا أَرَدْنَا إِلاَّ الْخَيْرَ. قَالَ وَكَمْ مِنْ مُرِيدٍ لِلْخَيْرِ لَنْ يُصِيبَهُ. إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَدَّثَنَا أَنَّ قَوْمًا يَقْرَءُونَ الْقُرْآنَ لاَيُجَاوِزُ تَرَاقِيَهُمْ وَايْمُ اللَّهِ مَا أَدْرِي لَعَلَّ أَكْثَرَهُمْ مِنْكُمْ ثُمَّ تَوَلَّى عَنْهُمْ فَقَالَ عَمْرُو بْنُ سَلَمَةَ: رَأَيْنَا عَامَّةَ أُولَئِكَ الْحِلَقِ يُطَاعِنُونَا يَوْمَ النَّهْرَوَانِ مَعَالْخَوَارِجِ.

Kutoka kwa ‘Amru bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulikuwa tumeketi mlangoni mwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd kabla ya Swalaah ya Alfajiri, akatoka nje. Tukaenda naye Msikitini. Kisha Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akatujia na kusema: “Je, Abuu ‘Abdir-Rahmaan ameshakuja kwenu?” Tukasema: “Hapana!” Akaketi hadi akatoka nje na alipotoka nje tukasimama. Abuu Muwsaa akamwambia: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan! Sasa hivi nimeona jambo Msikitini sijapatapo kuliona kabla, lakini sidhanii baya ila ni jambo jema.” Akasema: “Jambo gani?” Akasema. “Ukiendelea kuishi utaliona.” Akasema: “Nimeona Msikitini watu wameketi kwa mkusanyiko wa duara wakisubiri Swalaah. Katika kila duara alikuweko mtu na mikononi mwao mna changarawe. Mmoja wao akisema: “Semeni Allaahu Akbar mara mia!” nao wakisema “Allaahu Akbar!” mara mia. Kisha husema: “Semeni laa ilaaha illa-Allaah mara mia”! Nao husema “laa ilaaha illa-Allaah!” mara mia. Kisha husema: “Semeni Subhaana-Allaah mara mia!” Nao husema “Subhaana-Allaah!” mara mia. Akasema: “Je, umewaambia nini?” Nikasema: “Sikusema lolote, nilikuwa nasubiri nione utaonaje na nikisubiri amri yako.” Akasema: “Kwa nini usiwaambie wahesabu vitendo vyao viovu na kuwahakikishia kwamba vitendo vyao vyema havitopotezwa?”

Kisha akasogea nasi tukaenda hadi alipofikia moja kati ya maduara hayo akasimama na kusema: “Mnafanya nini?” Wakasema. “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hivi ni vijiwe tunavyohesabia takbiyr, tahliyl na tasbiyh.” Akasema: “Hesabuni vitendo vyenu viovu, kwani nakuhakikisheni kwamba vitendo vyenu vyema havitopotea hata kimoja! Ole wenu Ee Ummah wa Muhammad! Ni kwa haraka gani mnakimbilia kwenye uharibifu! Hawa ni Maswahaba wa Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wameenea. Hizi ndizo nguo zake ambazo bado hazijachakaa, na bakuli lake ambalo halijavunjika! Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mpo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama mnafungua milango ya upotofu!”

Wakasema: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hatukukusudia lolote ila khayr tu.” Akasema: “Wangapi waliokusudia khayr hawakuzipata?” Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia: ((Watu wataisoma Qur-aan, lakini haitovuka zaidi ya koo zao)) “Naapa kwa Allaah! Mimi sijui, lakini pengine mengi kati ya hayo yanatoka kwenu!” Baadaye akaondoka. ‘Amru bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tumewaona wengi kati ya watu hao wakipigana dhidi yetu katika siku ya Nahrawaan, wakiwa pamoja na Khawaarij.” [Sunan Ad-Daarimiy 206, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/11)]

 

 

Sababu Thelathini Na Moja:

 

Hakuna jambo lenye manufaa kwetu na lenye madhara isipokuwa ameshalibainisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hiyo ingekuwa Maulidi ni yenye kutufaa, basi angeliyathibitisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyosema:

 

مَا تَرَكْتُ مِن شَيءٍ يُقَرِّبُكُمْ إِلى الجَنَّةِ إِلاَّ أَمَرْتُكُمْ بِهِ، وَلاَ مِن شيءٍ يُبعدُكُمْ عَنِ النَّارِ إِلاَّ نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ

Sijaacha jambo lolote litakalokukurubisheni na Jannah isipokuwa nimekuamrisheni. Na wala lolote litakalokuepusheni na moto isipokuwa nimekuukatazeni)) [Hadiyth ya Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) As-Silsilah Asw-Swahiyhah (2866)]

 

 

Sababu Ya Thelathini Na Mbili

 

Wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu siku na mwezi aliozaliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Kuna waliosema ni Ramadhwaan, kuna waliosema ni Swafar, kuna waliosema ni Rabiy’ul-Awwal. Lakini Maswahaba hawakutilia himma kufuata au kuhakikisha kauli iliyo ya sahihi kabisa hata waone ni jambo muhimu kujua siku au mwezi alozaliwa ili washerehekee mazazi yake. Lilojulikana na kuthibitika, ni mwaka aliozaliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallaam) ambao ulikuwa unajulikana kuwa ni عام الفيل  (Mwaka wa tembo); ambao lilipotokea tukio la watu kutoka Yemen kina Abraha na tembo wao kuja kutaka kuvunja Al-Ka’bah Makkah, kwa amri ya Allaah, tembo hao waligoma kusogea kuelekea Al-Ka’bah, na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akawaangamiza watu hao na ndio sababu ya kuteremshwa Suwratul-Fiyl (Qur-aan: 105).

 

Imaam Ibnul Qayyim amesema:

"Hakuna ikhtilaaf kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amezaliwa Makkah na kwamba amezaliwa mwaka wa tembo." [Zaad Al-Ma'aad Fiy Hadyi Khayril-'Ibaad (1/76)].

 

Kipindi hicho tarehe za siku hazikuhesabiwa. Tarehe zilianza kuhesabika baada ya Waislamu kuhajiri kutoka Makkah kwenda Madiynah hivyo terehe na hesabu zikathibitika, na ndipo ikajulikana siku ya kufariki Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni tarehe 12 Rabiy’ul Awwal, siku ambayo wazushi wa Maulidi wanaitakidi kuwa ndio siku ya kuzaliwa! 

 

 

Sababu Ya Thelathini Na Tatu:

 

Shaytwaan anapendelea zaidi mwenye kutenda bid’ah kuliko mwenye kufanya maasi. Kwa sababu mwenye kutenda maasi, bila shaka nafsi yake inajitambua kuwa anafanya madhambi na huenda akarudi kutubia kwa Rabb wake. Lakini mwenye kutenda bid’ah, hubakia kudhania kuwa anatenda ‘amali njema (ilhali ‘amali ya bid’ah ni ya uzushi tu hata iwe nzuri vipi, kwani Rasuli kaishasema KILA bid'ah ni upotevu na KILA upotevu ni motoni). Hivyo shaytwaan humuandama mtendaji bid’ah na kumpambia 'amali zake aendelee kuamini kuwa anafanya mema.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

أَفَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا ۖ فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۖ

Je, yule aliyepambiwa uovu wa ‘amali yake akaiona ni nzuri (je, ni sawa na aliyeongoka?) Basi hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamwongoa Amtakaye. [Faatwir: 8]

 

Ndio maana utasikia hoja dhaifu za wanaosherehekea kusema” “Kuna ubaya gani kumswalia Mtume au kumsifu?” Au "Kwani nitaadhibiwa kwa kumswalia Mtume?" Au "Kwani yanayofanyika katika Maulidi si mambo yote yako katika dini kama kusoma Qur-aan, kumswalia Mtume n.k.?"

 

Na'am, hawatambui kuwa mtu haadhibiwi kwa kusoma Qur-aan, au kumswalia Mtume, au kula...lakini ataadhibiwa kwa kuzusha katika Dini.

 

 

Sababu Ya Thelathini Na Nne:

 

Katika baadhi ya beti au kauli za Maulidi kuna maneno yasiyoingia akilini uzushi na uongo mfano kutaja kuwa Aasiyah (aliyekuwa mke wa Fir’awn) na Maryam mama yake Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) walihudhuria mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)! Na beti nyingine kuwa mama yake pia alihudhuria siku ya

Na madai mengine ya uzushi na uongo kama yaliyomo kwenye beti mbalimbali za Maulidi.

 

 

Sababu Ya Thelathini Na Tano:

 

Yanayowasababisha Waislamu wanaosherehekea Maulidi ni:

 

1-Kufuata bila ya kuwa na ‘ilmu.

 

2-Kufuata matamanio ya nafsi ya kulipenda jambo bila ya kujali amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

   وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ

  na wala usifuate matamanio yakakupoteza na njia ya Allaah.   [Swaad: 26]

 

3- Ugumu wa kuacha mila na desturi

 

Ni sawa na watu wa kale walipokuwa wanalinganiwa na Rasuli wao waache upotofu na badala yake wafuate ya haki, walikanusha.  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾

Na wanapoambiwa: “Njooni katika yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli” Husema: “Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuongoka?     [Al-Maaidah: 104]

 

Wanaosherehekea Maulidi hali kadhaalika wanaponasihiwa waache uzushi hujibu: “Vipi tuache Maulidi na hali tumekulia nayo?”  Ni sawasawa na watu wa kale wakisema:  

بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ ﴿٢٢﴾

Bali wamesema: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi tunajiongoza kwa kufuata nyayo zao.”

 

وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ ﴿٢٣﴾

Na hivyo ndivyo Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake wenye starehe na taanusi: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao.” [Az-Zukhruf: 22-23]

 

4- Kukhofia kutokuungana na mkumbo wa Maulidi na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaonya:

 

 وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo. [Al-An'aam: 116]

 

5- Kudai kudhihirisha mapenzi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

6- Hudai kuwa ni bid'atun-hasanah (uzushi mzuri)

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

كل بدعة ضلالة

Kila bid'ah ni upotofu  

Imejumuisha kila aina ya bid’ah. Kama vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anavyojumuisha kila nafsi kuwa itaonja mauti Anaposema:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ  

Kila nafsi itaonja mauti.   [Al-'Imraan: 185]

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq

Share