Zakaah Ya Bidhaa Zenye Kuingia Na Kutoka

  SWALI LA KWANZA:


Assalaam Alaykum!

Nimetatizika kidogo na mambo ya zakaatul Mali. Naomba ufafanuzi katika mambo ya mahesabu. Vipi nafanya mahesabu ya Bidhaa zilizopo ofisini (Closing Stock). Mfano gharama ni:

1) Manunuzi (Purchasing Cost)    

2) Bima (Insurance)

3) Usafirishaji (Freight)

4) Malipo kwa serikali ( Duty & VAT)

5) Gharama za kuutoa mzigo ( Clearing Charges)

Ninapofanya stock taking kwa ajili ya Zaka:

a) Jee najumuisha ghaama zote au gharama zipi zijumuishwe kwa ajili ya kupata gharama kamili (Real Valuation cost of the stock).

b) Mzigo ambao upo njiani nishaununua (Goods on

Transit) tuujumuishe ndani ya hesabu au kwakua bado hatujaupokea tusiuingize. Nikipata majibu kwa kabla ya ramadhani nitafurahi sana mana twatarajia kutoa zaka. Mwaka wetu wa kifedha waishia Ramadhani. (The Financia year ends on Shaaban every year)

Twatanguliza shukran zetu za dhati.

SWALI LA PILI:

 UFAFANUZI WA SWALI LA MWANZO:

Asalaam Alykum,

Sisi twashughulika na Uagzaji wa bidhaa mbali mbali kutoka nje na kusambaza ndani ya nchi. Nyingi katika bidhaa zetu huchukua si zaidi ya miezi mitatu kumalizika.

Kiufupi kila mwezi twaingiza kama si contena moja basi mbili na juzi tu tumepokea contana tatu kwa pamoja. Hebu nifafanulie kipengele cha kupitwa na mwaka kwa biashara yetu hii kitatumikaje? Pia pesa iliyo benki ni mfano wa bdhaa mana mzunguko wake ni kutoka na kuingia, mara tumelipa wanaotuuzia mali (Creditors) mara nyengine twapokea kutoka kwa wateja wetu (Debtors). Hivyo balance ya benki ni vigumu kubakia mwaka mzima na vitu tunavyo agiza ni vigumu kubaki ofisini mwaka
mzima. Naomba ufafanuzi hapo! Wabillaahit Taufiiq!


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Moja katika masharti ya kukamilishwa kabla ya kutolewa Zakaah ni mali iliyopo ipitwe na Hawl (mwaka wa Kiislamu). Pia mali iwe ni yenye kumilikiwa wakati wa kutolewa Zakaah umilikaji uliotimia (complete possession) na tayari imeshatimia au kuvuka kiwango (Nisaab). Na Zakaah itahesabiwa pale mwisho wa Mwaka kwa kila kilichopo wakati wa kufunga mahesabu ambacho tayari kiko ndani ya milki ya mwenye kutoa Zakaah.

Hivyo kufafanua mas-ala yako ni kama ifuatavyo:

 

Shurti la kupitiwa na mwaka

Katika mali ya biashara ikiwa mwanzo wa mwaka yaani (Shawwaal kwa mfano uliotuletea) mali iliyopo tayari imefikia Nisaab (sawa na gramu 85 za dhahabu safi) basi ikimalizika mwaka (Ramadhaan) tunaangalia bidhaa iliyopo na pesa zilizopo Benki ambazo tayari zimo kwenye milki yenu na kisha kutoa Liabilities zote kama (madeni, malipo n.k) na kitakachobaki ndicho kitahesabiwa kutolewa. Bidhaa hutiwa thamani kwa mujibu wa thamani iliyopo (market value).

 

Tanbihi: Si lazima kuangalia nini kimeingia na kipi kimetoka wakati biashara inaendelea kinachotazamwa ni mwanzo wa mwaka je mali ilifikia kiwango? Na mwisho wa mwaka mali iliyopo yote ndiyo itakayotiwa katika hesabu ya Zakaah. Na kama mali yenyewe bado ni bidhaa basi gharama/thamani inayouzwa (market value) ndiyo kigezo cha kuangalia  na si gharama iliyonunuliwa (buying price). Hapa itategemea ikiwa mali hii katika mzunguko wake wa kibiashara haitopungua kiwango.

 

Hivyo mtaangalia bidhaa zenu zilizoko kwenye ghala kama zingeliuzwa wakati ule zingekuwa na gharama gani (inawezekana gharama hizi kuzidi au kupungua na bei iliyonuniliwa).

 

Na hapa tutawekea jedwali ndogo ya kuainisha vipi katika ulivyovitaja vitapaswa kutolewa/kutotolewa Zakaah

 

MALI/BIDHAA/LIABILITIES

ZINATOLEWA

HAZITOLEWI

BIDHAA ZILIZOPO DUKANI NA GHALANI

Ni bidhaa yenye kuongezeka na ipo kama ni mali

 

PESA ZILIZO BENKI NA MKONONI

Ni mali

 

MZIGO TUMESHANUNUA BADO UPO NJIANI

 

Kwa sababu bado hamjaumiliki kikamilifu(complete possession)

BIMA

Si sehemu ya matumizi (ingawa inategemea na BIMA yenyewe, pia na nchi kama ni lazima kuwa na BIMA ukiwa na biashara)

 

MALIPO YA SERIKALI VAT /INCOME TAX

Hujumuishwa katika hesabu ya kutoa Zakaah

 

GHARAMA ZA KUUTOA MZIGO

 

Ni sehemu ya matumizi

MISHAHARA

 

Ni sehemu ya matumizi

USAFIRISHAJI

 

Ni sehemu ya matumizi

MADENI (MNAYODAI)

Ikiwa yanatarajiwa kulipwa

 

MADENI (MNAYODAIWA)

 

Hamna uwezo wa kuyatolea

FAIDA (Profit)

Ni sehemu ya mali

 

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 





Share