Mume Au Mke Hawezi Tendo La Ndoa Kwa Zaidi Ya Miaka 5, Hukmu Ni Nini?

 

SWALI:

 

A friend asked me on the standpoint of Islam on the following issues:-

if a husband/ or wife has failed/ cannot perform the act of marriage to his lawful wife due to incapability (either health, accidents among the reasons) and this has persisted for a duration of more than 5 years and would like to raise up a family:-  Should the couple remain as pairs? What options are there if this situation persists?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu tendo la ndoa kwa mume au mke asiyejiweza. Uislamu uliokamilishwa na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam) umekuja kutazama maslahi ya mwanadamu. Uislamu wenyewe unakwenda sambamba na maumbile ya mwanaadamu.

 

Uislamu umekuja kumuondolea madhara klila mmoja wetu kwa njia tofauti. Katika hayo ni matatizo yanayopatikana kwa wanandoa pindi tatizo linapoibuka kwa njia moja au nyingine kama ugonjwa, madhara, na kadhalika. Katika hali ya ugonjwa au mume kutoweza kutenda tendo la ndoa, uamuzi unaachiwa mke mwenyewe. Ikiwa mke ameamua kubaki na mumewe ili kuendelea kumtunza na kumhudumikia basi atapata thawabu zake. Ama ikiwa hawezi kujizuia kwa kuwa hataweza kutimiziwa mahitaji yake ya kimwili, anaweza kwenda kwa Qaadhi na kulingana na sababu hizo ambazo zinaweza kumletea madhara makubwa zaidi. Qaadhi atamwachisha na baada ya eda ataweza kuolewa na mwingine.

 

Ama ikiwa mgonjwa ni mwanamke, basi mume anatakiwa amfanyie ihsani kwa kumbakisha mke huyo kama mke wake naye aoe mke wapili kwani sheria ya Kiislamu imempatia yeye fursa hiyo ya kuoa zaidi ya mke mmoja. Lau ataona uzito wa kuwaweka wake wawili kwa pamoja basi yeye amepatiwa ruhusa na sheria ya kumpatia talaka mkewe ili aweze kuoa mke mwengine. Hata hivyo, atakuwa na thawabu zaidi lau ataweza kumwangalia mkewe ambaye ni mgonjwa kwa kubaki naye.

 

Kwa muhtasari ni kuwa Uislamu umewaachia wanandoa uamuzi kunapotokea tatizo kama mme kutojiweza, ugonjwa, madhara na kadhalika.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share