Inafaa Kumuandikisha Agano Mume Asioe Mke Mwengine?

 

SWALI:

BISMILLAHI RAHMAN RAHEEEM.

ASSALLAM GHALAIKUM MY DEAR BROTHERS AND SISTERS.

FIRST OF ALL IT HAS BEEN WONDERFUL TO KNOW THIS SERVICE MAY ALLAH REWARDS ALL YOU FOR DOING THIS WONDERFUL JOB EVERY THING IN THIS WEB IN PERFECT AND VERY HELP FULL.

MY QUESTION IS;

MY FRIEND BEEN MARRIED FOR SOMETIME AND ON THE WAY SHE HAS BEEN UP AND DOWN WITH PROBLEMS THAT HER HUSBAND WANT TO TAKE A SECOND WIFE, SHE DOES NOT LIKE THE IDEA AND THEY END UP DIVORCE TWO TIMES IT HAS BEEN A YEAR SINCE THE SECOND DIVORCE, NOW HE WANT TO MARRY HER AGAIN AND SHE WANT HIM TO ENSURE THAT HE WILL NOT TAKE ANOTHER WIFE BY WRITING IS THIS PERMISIBLE? BY THE WAY THEY HAVE FIVE CHILDREN THEY HAVE DIFFERENT CULTURE AS WELL OTHER THAN HE WANT TO TAKE ANOTHER WIFE HE HAS BEEN VERY GOOD HUSBAND AND GOOD FATHER TO HIS KIDS JAZAKA LLAH KHEIR WASSALLAM GHALAIKUM.

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo zuri kuhusu uke wenza. Uke wenza ni jambo ambalo limetajwa katika Qur-aan, Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ni mwenendo wa Manabii waliotangulia.

Allaah Aliyetukuka Anasema wazi kabisa:

Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu” (4: 3). Dada zetu wana matatizo inapokuja kuwa mumewe anataka kuoa mke mwengine ili kujikinga na mambo mengine. Hii ni fursa nzuri kwa mke mwenyewe kumsaidia mumewe ili kutekeleza jambo hili ambalo pia ni muhimu. Ni sikitiko kuwa dada badala ya hivyo ndio anafanya maisha ya ndoa yawe magumu kiasi ambacho jambo baya zaidi linatokea kwa kuachana kisha baadaye yanakuja majuto. Wapo wengine wanakhiari waume zao wawe na vimada kuliko kuoa mke wa pili.

Kitu cha muhimu katika suala hilo ni kuhakikisha kuwa mume wako amekutimizia mahitaji yako ya kimsingi katika hali ya uanandoa. Kinyume cha kufanya hivyo tunaingia katika mashaka na matatizo.

Haifai kwa mwanamke kuweka sharti katika ndoa, jambo ambalo litakuwa kinyume na sheria ya Dini na hilo sharti ambalo anataka mtalaka wake alikubali ni kinyume hivyo halitakubaliwa.

Ni ajabu kwa huyo mke kupata mume ambaye amejali maslahi yake kwa kumtazama kwa njia nzuri pamoja na watoto walio nao au waliozaa pamoja. Mume aina hiyo ni adimu na juu yake kupiga moyo konde na kujihimiza katika kumsaidia mumewe kwa njia zote zinazowezekana. Yaonyesha kuwa hawa wanandoa ni watu wenye kupendana kwani kila wanapoacha wanarudiana tena. Hata hivyo, tufahamu kuwa wakirudiana sana ndio mara ya mwisho, wakiachana tu hawataweza kurudiana tena kwani talaka ya tatu itakuwa imetoka. Kuweza kurudiana mpaka mke aolewe na mume mwingine, kisha aachwe. Hiyo itakuwa ni shida kwa wote.

Ni ajabu pia kutuambia kuwa utamaduni wao ni tofauti. Sijui ulikuwa unamaanisha nini kwani wote ni Waislamu na utamaduni wao moja kwa moja utakuwa ni Uislamu. Inaonyesha mmoja wao ameshika zaidi utamaduni wa kiukoo au kikabila zaidi kuliko Uislamu na hilo huwa mara nyingi linaleta matatizo yaliyo mazito. Tujivue katika hayo ili tupate kusalimika.

Tunawaombea kila la kheri wanandoa hao wawili.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share