Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 09

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam - 09

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 9 Linaloeleweka Vibaya

 

 

Uislamu ni dini ya kibaguzi, ni dini hasa ya Waafrika kwa sababu:

 

  • Nation Of Islam 'Taifa la Kiislamu'[1]linafuata daraja kuu ya watu weusi

 

  • Nation Of Islam ‘Taifa la Kiislamu’ linatambua Allaah kuwa ni mtu mweusi

 

Moja wapo ya masuala yanayoeleweka vibaya kuhusu Uislaam kwa karne ya ishirini ni kule kuita ‘Taifa la Kiislamu’ kuwa ni jamii ya Waislamu, au kwa ufafanuzi zaidi: jamii ambayo inanyenyekea kwa Allaah kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. ‘Taifa la Kiislamu’ ni njia ya maisha iliyofanywa na watu iliyoazima aina fulani za Uislaam na kuzichanganya pamoja na mambo ya uzushi yaliyo mengi na uongo ili kufikia uamuzi wao wa leo.

 

Inatosha kueleza kwamba Taifa la Kiislamu limepotoka kwa njia mbili. Kwanza, wanakataa msingi wa Uislaam kwa kufanyiza simulizi ambayo Allaah anachorwa kwa mfumo wa mtu mweusi. Kwa mujibu wa machapisho yao ya kwenye mtandao, tunaona kwamba ‘Taifa la Kiislamu’ linaamini kwenye:

 

…Allaah mmoja (Allaah) na kwamba Allaah (Mungu) alijitokeza kwa njia ya Mwanaadamu kupitia kwa Mkuu W. Fard Muhammad, Julai, 1930, huyu ni Masihi wa Wakritso na ‘Mahdi’ wa Waislamu aliyekuwa akisubiriwa kwa muda mrefu.

 

 Hata hivyo, Allaah Anaeleza ndani ya Qur-aan:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

 

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-An’aam: 103]

 

Pia ‘Taifa la Kiislamu’ linadai kwamba watu weupe ni ‘mashetani’, na kwamba watu weusi kwa ujumla ni bora kuliko makabila mengine. Hata hivyo, Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya khutba ya kuaga ya Rasuli wa Allaah, tunaona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Watu wote wanatokana na Adam na Hawa, Muarabu hana ubora juu ya asiye kuwa Muarabu wala asiye kuwa Muarabu hana ubora juu ya Muarabu, pia mweupe hana ubora juu ya mweusi wala mweusi hana ubora juu ya mweupe – isipokuwa kwa Mcha wa Allaah na mwenye matendo mazuri.

 

Kuna dhana nyingi nyengine ambazo ‘Taifa la Kiislamu’ linakamatana nazo zinazolipeleka nje ya Uislaam. Ni ajabu kuona kwamba mnamo miaka ya kati ya 1970, walio wengi walitambua makosa yake na kubadilika kuingia kwenye Uislaam wa kweli. Lakini kuna kipande cha kikundi, ambacho bado kipo hai.

 

 

.../10

 

 

 


[1]

Maneno ya ‘Taifa la Kiislamu’ yaliyotumika hapa sio kwa Taifa halisi linalofuata Uislamu kwa misingi ya Qur-aan na Sunnah. Isipokuwa, ‘Taifa la Kiislamu’ lililokusudiwa hapa ni Jumuiya ya Waislamu weusi wanaoishi Marekani wanojulikana kama Nation Of Islam lilikokuwa likiongozwa na Elijah Muhammed, ni watu wasioelewa misingi sahihi ya Uislaam na Wanachuoni wamesema hao si Waislamu. [Mfasiri]

 

 

Share