Chila-1

Vipimo
Mchele 2 Vikombe
Tui 2 Vikombe
Sukari 1 Kikombe
Maziwa ½ Kikombe
Hamira 1 Kijiko cha chai
Hiliki Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka mchele na maji kwa muda mpaka ulainike kiasi.
- Chuja mchele kisha saga vitu vyote vilivobali katika mashine ya kusagia (Blender) huku ukimimina tui kidogo kidogo mapaka limalizike
- Mimina kwenye bakuli kisha acha mpaka uumuke
- Weka chuma cha kuchomea katika moto, kisha chota upawa wa mchanganyiko huo umimine kwenye chuma cha kuchomea huku ukiuzungusha utandazike. Choma katika moto wa kiasi.
- Ukishabadilika rangi tu chini na ukafanya matundu matundu juu utoe na weka kwenye sahani zikiwa tayari.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Bismillahi Rahaman
Bismillahi Rahaman Raheem
Asalaam Alykum, Tamu na rahisi kufanya shukran kwa kazi bora jazza zenu ziko kwa Mola Mwenyezi Inshallah.
Jazzak Allahu Khery.