Aayah Katika Suwrah Faatwir إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء Ina Maana Gani?

 

Aayah Katika Suwrah Faatwir

 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء

 

Ina Maana Gani?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

I have a question that maybe most of the people want to know  about. Its about the Quran . Well I know arabic and I can read the Quran but I dont understand what it means i just read. Sometimes I  wonder why is this Surah brought down. 

 

I  read an article saying that one man was about to die, the Malaika was there want to take out his roh, so there was  someone with him in the room, so the Malaika told the person can you  move because i want to take out his roh, the person said no, I cant  leave him, he was there for me  and I cant leave him, so the Malaikas struggled to take out his roh while the person is there watching. At the end I knew that that person is the Quran, its the one  who will be there for you because it will tell you that you didnt leave me and I wont leave you.

 

Ufafanuzi Uliohitajika Kutoka Alhidaaya Ili Swali Liweze Kujibiwa:

 

Tunahitaji kujua kama uliyotaja ni Tafsiyr ya Suwrah au Aayah, na kama ndio, tafadhali tujulishe ni Suwrah gani na Aayah gani ili tuweze kuhakikisha usahihi wake na kuweza kujibu Swali lako In shaa Allaah.

 

Majibu ya muulizaji ni:

 

Assalamu Alaikum

 

The Aayah that I really want to know is Suwarah Faatwir, Aayah 28  

 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء  

Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. [Faatwir:28].  

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Baada ya kufanya utafiti wa aya hiyo hatukuona maelezo hayo uliyotaja kuhusu mtu aliyekuwa anakata roho, bali maelezo yenye maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo: 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء

Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. [Faatwir: 28]

 

Nao ni wale wenye elimu na wenye kumkhofu Allaah kama Apasavyo kukhofiwa kwa sababu kila anapokuwa mtu ana elimu ya kumtambua Rabb Mtukufu, Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi, Mwenye sifa zilizokamilika na Mwenye majina matukufu ndipo anapokuwa anazidi kuwa na khofu Naye.

 

Ibn 'Abbaas amesema kuhusu aya hii:

 

"Miongoni mwa waja wanaomjua Ar-Rahmaan ni yule ambaye hamshirikishi na chochote katika kumuabudu. Na ni mwenye kukubali yaliyo halali Aliyohalalisha na kukubali kuepukana na yaliyo haramu Aliyoharamisha Allaah  Subhaanahu wa Ta'aalaa. Ni mtiifu wa amri zote na ana yakini kuwa ataonana Naye na kuwa atasimamishwa mbele Yake kuhesabiwa vitendo vyake".

 

Hasan Al Basriy amesema:

 

"Mtu mwenye elimu ni yule mwenye kumkhofu Ar-Rahmaan kwa mambo yasiyoonekana, na mwenye kupenda yale ambayo Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa Anamtaka ayafanye na mwenye kujiepusha na yale ambayo yanamghadhibisha Allaah" Kisha Hasan Al Basriy akasoma:

 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴿٢٨﴾

Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria. [Faatwir: 28] 

 

Sufyaan Ath-Thawariy amesimulia kutoka kwa Abu Hayyaan At-Taymi kutoka kwa mtu aliyesema: "Iilikuwa ikisemekana kuwa wenye elimu ni aina tatu; (kwanza) mwenye kumjua Allaah  Subhaanahu wa Ta'aalaa na amri Zake (pili) mwenye kumjua Allaah  Subhaanahu wa Ta'aalaa lakini hajui amri Zake (tatu) mwenye kujua amri Za Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa lakini hamjui Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa .   

 

Mwenye kumjua Allaah  Subhaanahu wa Ta'aalaa na amri Zake ndiye mwenye kumkhofu Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa na mipaka Yake pamoja na aliyofaridhishiwa. Mwenye kumjua Allaah  Subhaanahu wa Ta'aalaa lakini hajui amri Zake ni mwenye kumkhofu Allaah lakini hajui mipaka yake na aliyofaridhishiwa. Mwenye kujua amri za Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa lakini hamjui Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa ni mwenye kujua mipaka na aliyofaridhishiwa lakini hamkhofu Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa  [Ibn Kathiyr :8:145-146]

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share