Kuswali Sunnah Kabla Ya Swalaah Ya Magharibi Inafaa?

 

 

Kuswali Sunnah Kabla Ya Swalaah Ya Magharibi Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI

 

Asalam alaykum warahmatullah wabarakatuh

 

mimi swali langu ni hili hapa nina mama yangu anaomba jibu lenu anasema huwa anasali sala ya sunna kabla maghrib na baada ya maghrib na kaambiwa haifai lakini bado anaendlea sasa je ni makosa au aendelee tu mana yuko katika njia panda hajui afanye nini? Wabillah taufiq in shaa Allah Allah atakupeni wepesi wa kujibu maswali yetu yote ameen
 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakuna makatazo ya kuswali Sunnah kabla ya Magharibi au baada ya Maghrib bali inapendekezeka kufanya hivyo. Ila huenda imefahamika kwa aliyemkataza kuswali, kuwa ni kabla ya kuadhiniwa Magharibi, kwa maana baada ya Swalaah ya Alasiri. Ikiwa hivyo basi itakuwa haifai  kwani wakati huo ni miongoni mwa nyakati ambazo  makruwh (zinazochukiza kuswali), hivyo hakuna Swalaah ya Sunnah. Lakini baada ya kuadhiniwa Magharibi inafaa kuswali Sunnah ambayo inajulikana kuwa Sunnah Ghayr Muakkadah (Sunnah isiyosisitizwa).

 

Tafadhali ingia katika kiungo kifutacho upate ratiba ya Swalaah za Sunnah zote ambazo zimetajwa pia hizo Sunnah mbili za kabla ya Magahribi na baada yake.

 

Swalaah Za Sunnah Muakkadah (Zilizosisitizwa) Na Ghayr Muakkadah (Zisizosisitizwa)

 

 Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share