Vipi Kutia Niyyah Swalaah Za Qiyaamul-Layl?
Vipi Kutia Niyyah Swalaah Za Qiyaamul-Layl?
SWALI:
Asalama alykom warahmatulah wabarakatuh, mie nilikua nina tatizo dogo kua nimesoma na nimefahamu namna ya kusali sala za mwisho wa kundi la Ramadha (laylatullkadr) Lakini sijaona nia inatiwa vipi kidogo wengine hatui ndio tunajifunza. Kwa hiyo nilikua ninaomba unifahamishe vipi unatia nia ya sala hizi. Pia nia ya sala ya tahajud. Ahsante sana kwa muda wako Jazakah Allah fih.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tumepokea Swali lako. Tunakuomba mara ya pili pindi upendapo kutuma Swali tafadhali weka Maudhui (subject) ieleweke vizuri kama tulivyoweka sisi hapo juu.
Jibu ni kwamba, niyyah yoyote ya ‘ibaadah huwekwa moyoni na haitamkwi. Kwa hiyo unapoamka usiku ukatawadha, ukasimama katika mswala au kwenda msikitini kuswali Taraawiyh itakuwa tayari umeshaweka niyyah yako moyoni. Hivyo ndivyo ilivyokusudiwa.
Hapa tunatoa mfano wa kutia niyyha katika mambo yasiyo ya ‘ibaadah. Mfano, mwizi anapotaka kwenda kuiba, huamka usiku kimya kimya, akachukua hazina zake za kufungulia milango, kisha akatoka kwenda kuiba ikiwa ni katika nyumba ya mtu au dukani. Utafahamu kuwa huyu tayari alikwisha weka niyyah moyoni mwake kwenda kuiba na hakusema kwa sauti "Leo nakwenda kuiba". Tunatumai kwa mfano huu utakuwa umeelewa vizuri vipi imekusudiwa niyyah kutia moyoni.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate faida ziyada:
Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Bid’ah Bali Mahali Pake Ni Moyoni
Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Katika Akili Na Dini
Swalaah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Niyyah?
Na Allaah Anajua zaidi