Zakaatul-Fitwr: Maisha Yetu Ni Duni Je, Inatupasa Kutoa Zakaatul-Fitwr?

 

Maisha Yetu Ni Duni Je, Inatupasa Kutoa Zakaatul-Fitwr?

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalamu ' Alaykum wa Rahmatullah Wabarakatuh.

Sifa zote njema ni zake Allah Subhanahu Wata'ala.

 

Mie ni mwanamke nimeolewa na nimejaaliwa kupata mtoto mmoja hadi sasa. Katika familia yetu tupo watu watatu (yaani mie, mume wangu na mtoto). Kiuchumi mie ndio ninayefanya kazi na kutazama majukumu yote ya familia yangu, mume wangu hana kazi. Na maisha yetu ni ya hali ya chini kabisa. Suali langu ni hili, imefika Eid-ul fitr hatukuwa na pesa kwa ajili ya zakaatul fitr, je itanipasa nifanye nini? Na nini hukumu yangu ya kutotowa zakaatul fitr?

 

Nia yetu ilikua tuote ila hatukujaaliwa kwani tulikua na madeni ndio tukalipa kidogo na bado madeni hayajesha. Naomba mnifafanulie la kufanya ili tupate radhi za mola wetu mlezi.

 

Allah Subahanahu Wata'ala atakulipeni mema na atkuepusheni na adhabu duniani na akhera, amiin.

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Mwanzo twakupongeza kwa juhudi zako nzuri katika kutazama familia yako.

 

Pili, ni nasaha kwako uzungumze na mumeo kwa njia iliyo nzuri na umueleze kuhusu umuhimu wa kufanya kazi hata ikiwa inaonekana duni maadamu ni ya halali kwa muruwa na heshima ya Muislamu mwanamme ni kufanya kazi na kusaidia familia yako.

 

Baada ya hayo ni kuwa Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

 

Allaah haikalifishi nafsi yeyote ila yaliyo sawa na uweza wake” (Al-Baqarah: 286).

 

Ikiwa nia kweli ni ya kutoa Allaah Aliyetukuka Anakupatia thawabu hiyo ya kutoa japokuwa hukuwa na cha kutoa. Hakika ni kuwa nyinyi ndio wa kupatiwa Zakaatul Fitwr kutoka kwa Waislamu wengine.

 

Hata hivyo, kama mtapata Zakaah hiyo kutoka kwa Waislamu na ikazidi mahitaji yenu itabidi nanyi mutoe kuwapatia Waislamu wengine.

 

Tafadhali  bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na faidi zaid:

 

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share