Mtoto Anayezaliwa Anapasa Kuadhiniwa Wakati Gani? Na Je Apewe Jina Anapozaliwa tu Au Baada Ya Siku Kadhaa?

 

 

SWALI:

 

asalam aleykum warahmatulahi wabarakatuh ama baada ya salaam ndugu zangu waislam nashukuru kupata wasaa huu nami ndugu yenu kuuliza swali na natumai kwa uwezo wa  allah subhana wa taalah mtanielewa na kunijibu kwa ufasaha ndugu yenu.

 

 swali langu ni mtoto akizaliwa anapewa jina baada tu ya kuzaliwa au baada ya siku kadhaa na ningapi  na pia huadhiniwa baada ya kupewa jina au kabla  ni hilo swali langu ndugu zangu waislam na kwa mara nyengine tena namshukuru allah subhanah wataalah kwa kunijaaliauzima na afya njema na kuniwezesha kuwasiliana nanyi ndugu zangu  ahsanteni wabilahi taufiq

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wakati wa kuadhiniwa Mtoto na kupewa jina. Ama kuhusiana na kuadhiniwa mtoto anatakiwa atekelezewe hilo pindi tu anapozaliwa ili maneno ya kwanza atakayo yasikia akiingia hapa duniani ni utukufu na majina ya Allaah Aliyetukuka na maneno mazuri na mema.

 

Ama kususiana na kupatiwa jina mtoto aliyezaliwa ni kwa mfumo ufuatao kwani suala hilo lina wasaa mkubwa. Mifumo iliyotumiwa ni:

 

1.     Kupatiwa jina anapozaliwa tu, kama alivyompatia jina Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) mtoto wa Umm Sulaym na Abu Twalhah (Radhiya Allaahu ‘anhuma).

 

2.     Kupatiwa jina siku ya saba pamoja na kumfanyia mambo mengine kama alivyoashiria Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam).

 

3.     Kumuekea jina utakalompa hata kabla ya kuzaliwa.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

 

Vipi Kuadhiniwa Mtoto?

 

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah

 

Yanayopasa Kufanywa Na Mwenye Mimba Na Baada Ya Kuzaa

 

Kufanya Aqiyqah Ni Lazima Au Sunnah?

 

'Aqiyqah Afanyiwayo Mtoto Mchanga

 

Umri anaotakiwa mtoto mchanga kunyolewa nywele

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share