Biskuti Za Tangawizi

Biskuti Za Tangawizi

 

Vipimo

                                  

Unga - 2 Vikombe

Cocoa ya unga -  1 Kijiko cha supu

Sukari ya hudhurungi  - 1 Kikombe

Siagi  -   ¾ Kikombe

Yai  -   1

Molasses - ¼ Kikombe

Baking soda - 2 vijiko vya chai

Mdalasini wa unga -  1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi -  1 kijiko cha supu

Karafuu ya unga -  ½ kijiko cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai  

Vanilla  ½ kijiko cha chai

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
  2. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
  3. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
  4. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
  5. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
  6. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
  7. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza  kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
  8. Tengeneza viduara vidogo vidogo.

 

           

9-Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka

         

10-Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.

11-Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.

12-Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.

13Panga kwenye sahani tayari kuliwa.

 

 

 

 

 

Share