Hilaal: Kufuata Mwezi Wa Kitaifa Au Wa Kimataifa, Zamani Walipataje Khabari Za Mwandamo?

 

Hilaal: Kufuata Mwezi Wa Kitaifa Au Wa Kimataifa,

 

Kupishana Masaa, Na Je, Zamani Walipataje Khabari Za Mwandamo?

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

SWALI:

 

Assalaam alaikum,

Nimekuwa njia panda hasa ikifika wakati wa kuandama mwezi, kwani tumekuwa tukisikia miongozo mbalimbali juu ya muandamo wa mwezi kutoka kwa masheikh tofauti na kila mmoja akishikilia upande wake, swali

1.  ni muandamo gani wamwezi tunaotakiwa kuufuata hasa? Je ni ule unaoonekana maeneo ya kwetu? Au ule wa kimataifa popote utakapo onekana duniani?

 

2. Katika hii dunia tumetofautiana kimasaa utakuta nchi moja hadi nyingine wametofautiana masaa 8 hadi 12. Je inakuwaje pale watu wanakuwa kwenye viwanja vya arafa na wao unakuta wapo nyuma kimasaa?

 

3. Kukua kwa teknolojia hivi karibuni kumerahisisha mambo mengi hasa kuhusu kupashana habari juu ya muandamo wa mwezi, je ilikuwa vipi kipindi cha nyuma wazee wetu walikuwa wanapata wapi habari juu ya huu mwezi wa kimataifa? Na jee nitakuwa makosani nikifuata muandamo wa mwezi wa hapa nilipo ambao unatofauti ya siku moja na huu wa kimataifa, na hivyo kunionyesha kuwa siku ya tarehe 9 itakuwa ijumaa na sio alkhamis?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Hakika swali hili limekuwa na mzozano mkuu katika ulimwengu kila sehemu. Na swali hili tumelijadili sana katika tovuti hii.

Kwa mukhtasari ni kuwa ipo misimamo miwili kuhusiana na mwandamo wa mwezi. Kuna msimamo wa kufunga pindi uonekapo popote duniani, na ule wa kufunga kwa kuonekana katika nchi anayoishi mtu. Na misimamo yote miwili ina kundi kubwa la Wanachuoni wenye kuiunga na wana dalili zao.

 

Lakini msimamo wenye nguvu zaidi kwa dalili ni kufuata mwezi uonekapo popote ulimwenguni maadamu umeyakinishwa na Muislamu.

 

 

Ama kuhusu tofauti hiyo ya masaa uliyotaja, si kubwa kutufanya sisi tutofautiane katika kufunga na kufungua. Kwa tofauti hiyo bado watu wanaweza kupata habari na kufunga bila ya tatizo lolote.

 

 

Ama kuhusu mawasiliano hapo zamani kulikuwa hakuna ila tu yalikuja baada ya kupatikana kwa simu. Kwa ajili hiyo watu walikuwa wakitegemea muandamo wao kwa kukosekana mawasiliano hayo. Mawasiliano yalipopatikana msimamo huu wa mwandamo wa kimataifa ambao umesimamiwa kwa muono wa Imaam Abu Haniyfah, Maalik na Ahmad bin Hanbal kufuatwa.

 

 

Kwa kuwa misimamo miwili imekubaliwa na Wanachuoni kuwa inaweza kufuatwa, hata hivyo, ni bora zaidi kufuata mwandamo wa kimataifa ambao tunaona dalili zake na mantiki yake ina nguvu zaidi.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi

 

Tunaambiwa Wanaofuata Mwezi Wa Kimataifa Wamekosea Na Walipe Swawm Je, Ni Sawa?

 

Ni Sawa Kumfuata Mume Kwa Msimamo Wa Mwezi Wa Kitaifa Japokuwa Alikuwa Akifuata Unapoonekana Popote Duniani?

 

Mwandamo Wa Mwezi – Waislamu Wote Duniani Wafunge Siku Moja Na Kula ‘Iyd Siku Moja ?

 

Kuandama Mwezi – Afuate Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?

 

Mwandamo Wa Mwezi, Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?

 

Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu Je, Tulipe Siku Hiyo?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share