Al-Lajnah Ad-Daaimah: Majini Wanajua Elimu Ya Ghayb?

 

Majini Wanajua Ghayb?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, majini wanajua elimu ya ghayb?

 

JIBU:

 

Elimu ya ghayb ni makhsusi ya Ar-Rubuwbiyyah (Tawhiyd ya Uola), kwani hakuna ajuaye ya ghayb ya mbingu isipokuwa Allaah Ta’aalaa Ambaye Anasema:

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ  

59. Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu.  [Al-An’aam: 59]

 

Na Anasema Jalla Jalaaluh:

 

لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah (Pekee). Na wala hawatambui (ni) lini watafufuliwa.” [An-Naml: 65]

 

Basi majini hawajui ya ghayb na dalili ni kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿١٤﴾

Basi Tulipomkidhia mauti, hakuna kilichowajulisha kifo chake isipokuwa kiumbe cha ardhi (mchwa) akila fimbo yake.  Basi alipoanguka ikawabainika majini kwamba lau wangelikuwa wanajua ya ghayb, basi wasingebakia katika adhabu ya kudhalilisha. [Sabaa: 14]

 

Kwa hiyo atakayedai kuwa anajua ya ghayb basi yeye ni kafiri. Na yeyote anayeamini madai haya basi yeye ni kafiri pia kwa sababu anakadhibisha Qur-aan.

 

Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. (18645) Juz: 2 Uk.6]

 

 

 

Share