Mikate Ya Hamira Na Ufuta Ya Kuoka (Baked)

Mikate Ya Hamira Na Ufuta Ya Kuoka (Baked)

Vipimo 

Unga -  4 mugs (vikombe vikubwa)

Hamira - 1 Kijiko cha kulia

Mtindi (Yoghurt) - 1 kijiko cha kulia

Yai -  1

Samli - 1 kijiko cha kulia

Tui la nazi au maziwa - 1 ½ mug (takriban)

Chumvi - kiasi

Ufuta - kiasi 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika     

  1. Katika bakuli au mashine ya kukandia unga, weka vitu vyote isipokuwa ufuta.
  2. Kanda vizuri mpaka uwe laini.
  3. Fanya madonge saizi upendayo yasiwe madogo sana.
  4. Sukuma kila donge kisha pakaza samli kidogo ukunje kama paratha (chapati za mafuta).
  5. Pakaza siagi au samli katika treya ya oveni. Panga mikate, kisha iache iumuke.
  6. Piga yai moja vizuri kisha kisha upakaze kwa brush juu ya mikate na nyunyizia ufuta.
  7. Oka (bake) katika oveni moto wa kiasi. Ikikaribia kuiva, iwashie moto wa juu kidogo igeuke rangi na kumalizikia kuivisha.
  8. Epua weka katika sahani, pakaza samli ikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share