Paratha Mkate Kusukuma 1

Paratha Mkate Kusukuma 1

 

Vipimo   

 

Unga vikombe 4

Samli vijiko 2 vya kulia

Maji kiasi

Chumvi

Samli ya kupakia katika donge na ya kukaangia.

 

 

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

 1. Weka unga katika bakuli, tia chumvi na samli vuruga uchanganye unga.
 2. Weka maji kidogo kidogo uchanganye uwe donge lisiloganda mkononi.
 3. Kanda vizuri kisha liponde ponde kwa nyuma ya vidole unyunyuzie maji kidogo.
 4. Funika kwa karatasi ya plastiki uache muda robo saa.
 5. Rudi kuchanganya kisha ukande vizuri mpaka ulainike.
 6. Funika tena uache muda wa nusu saa uzidi kuwa laini.
 7. Ukusanye vizuri kisha kata madonge kiasi. Weka tena muda dakika chache madonge yajitawanye yawe wepesi kusukuma.
 8. Sukuma donge moja na utandaze kubwa kisha pakaza samli iliyoyayushwa.
 9. Nyanyua unga upige pige kwenye kibao au baraza ya jikoni uzidi kutandazika kisha zungusha liwe donge.
 10. Acha tena muda wa dakika chache, Sukuma uchome upande mmoja kwanza, kisha geuza uchome na utie samli na kupika mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi.
 11. Epua weka katika sahani na ukusanye hapo hapo ukiwa umoto na uvuruge kidogo kwenye sahani. Malizia madonge yote.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share