Kuku Wa Kuchoma Na Spices Ya Montreal (Canada)

Kuku Wa Kuchoma Na Spices Za Montreal

 

Vipimo: 

Kuku - 2

Bizari ya Montreal ya kuku - 5 vijiko vya kulia

Mtindi (yoghurt)  - ½  kikombe

Chumvi  - kiasi

Ndimu - 1 kamua

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Kata kuku mapande manne, muoshe vizuri kwa siki na chumvi. Mchuje maji kisha weka katika bakuli.
  2. Changanya mtindi na viungo vyote, mimina katika kuku mchanganya vizuri uroweke kuku kwa muda wa masaa 3 au zaidi.
  3. Paka mafuta katika treya unayochomea kuku, weka kukua uchome (grill) kwa moto kiasi huku unamgeuza mpaka aive.
  4. Epua akiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share