Du’aa Baada Ya Adhana

Du’aa Baada Ya  Adhana

SWALI:

Asalam aleikum warahmatullah wabarakatuh, naombeni mnitumie dua ya baada ya Adhana in sha Allah

 


JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Du’aa iliyothibiti baada ya adhana ni:

اللّهُـمَّ رَبَّ هَذِهِ الدّعْـوَةِ التّـامَّة وَالصّلاةِ القَـائِمَة آتِ محَـمَّداً الوَسيـلةَ وَالْفَضـيلَة وَابْعَـثْه مَقـامـاً مَحْـمُوداً الَّذي وَعَـدْتَه  

Allaahumma Rabba haadhihi da’watit taamah, wasw-swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.

“Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) al-Wasiylah (cheo, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kusifiwa, ambayo Umemuahidi.”

Na Allaah Anajua zaidi

Share