225-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 225: لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah225:
llaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini..
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾
225.
Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ
“Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi…” (2:225) imeteremshwa kutokana na vile mtu kuapa: “Hapana wa-Allaahi, Ndio wa-Allaah.” (Yaani kuapa apa kila mara). [Amehadithia ‘Aaishah (رضي الله عنها) na ameipokea Al-Bukhaariy]
Hadiyth kama ilivyothibiti:
عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أُنْزِلَتْ هَذِهِ الآيَةُ : ((لاَ يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ)) فِي قَوْلِ الرَّجُلِ: لاَ وَاللَّهِ، وَبَلَى وَاللَّهِ.
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Aayah hii
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ
“Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi” kuhusu kauli ya mtu (kusema kwake mara kwa mara): “Hapana wa-Allaahi, ndio wa-Allaahi. ” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]