Imaam Ibn Baaz: Nasiha Kwa Waislamu Kupokea Ramadhwaan Kwa Tawbah Ya Kweli Na Kujifunza ‘Ilmu Ya Dini Yao
Nasiha Kwa Waislamu Kupokea Ramadhwaan
Kwa Tawbah Ya Kweli Na Kujifunza ‘Ilmu Ya Dini Yao
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Nasiha yangu kwa Waislamu wote ni kwamba wamche Allaah (Jalla wa’Alaa), na waupokee mwezi wao kwa tawbah ya kweli kutokana na madhambi yote, na watafute ‘ilmu kujifunza yanayohusiana na Dini yao na wajifunze hukmu za Swawm zao na hukmu za Qiyaam chao (Kisimamo cha usiku kuswali) kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Allaah Akimtakia khayr mja, humpa ufahamu wa Dini.“ [Al-Bukhaariy]
[Fataawa Shaykh Ibn Baaz]