Imaam Ibn Baaz: Kutazama Mswahafu Bila Ya Kutamka Kitu

 

Kutazama Mswahafu Bila Ya Kutamka Kitu

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Hakuna ubaya kutazama Qur-aan bila ya kuisoma kwa ajili ya kuzingatia na kutia akilini na kuifahamu maana, lakini haitohesabiwa kuwa ni kuisoma wala hatopata mtu fadhila za kusoma isipokuwa ikiwa ataitamka Qur-aan hata ikiwa hatomsikia aliye karibu naye kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni kiombezi kwa Swahibu wake)) [Muslim]

 

 

Na alokusudia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni ‘Swahibu wake’ ni wale ambao wanaifanyia kazi kama vile ilivyotajwa katika Hadiyth nyingine. Na  akasema:

((Atakayesoma herufi moja katika Qur-aan atapata kwayo hasanah (jema) moja, na hasanah  moja ni sawa na kumi mfano wake)) [At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy].

 

 

Wala hatohesabiwa kuwa ni kuisoma isipokuwa aitamke kama walivyonukuu Ahlul-‘Ilm (‘Ulamaa).

 

 

[Fataawaa Manshuwrah fiy Mawqi’ Rasmiy li ibn Baaz]

 

 

 

Share