Imaam Ibn Baaz: Ramadhwaan: Usiku Wa Laylatul-Qadr Hubadilika Kila Mwaka

 

Usiku Wa Laylatul-Qadr Hubadilika Kila Mwaka

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Layaltul-Qadr hubadilika katika masiku ya kumi na si kwamba kuna siku maalumu katika nyusiku hizo. Huenda ikawa ni usiku wa 21 au 23 au 25 au 27 ambazo ni aghlabu zinategemewa na huenda pia ikwa usiku wa 29, au hata pia unaweza kuangukia masiku ya shafawiy (20, 22, 24, 26, 28).

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akihusisha nyusiku hizi kwa kuongezea na kujitahidi (katika ‘ibaadah) ambazo hakuwa hakizitekeleza katika masiku ya 20 ya mwanzo (ya Ramadhwaan) na Maswahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na Salaf walikuwa nao wakihuisha nyusku hizi na kujitahidi mno katika aina mbali mbali za ‘amali njema.”

 

 

[Al-Ikhtiyaraat Al-Fiqhiyyah, uk. 243]

 

 

Share