Shaykh Fawzaan: Mwenye Hedhi Kugusa Qur-aan Au Aayah Katika Simu Za Mkononi
Mwenye Hedhi Kugusa Qur-aan Au Aayah Katika Simu Za Mkononi
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya mwanamke mwenye hedhi kugusa maneno ya Qur-aan ambayo yamo katika simu za mkononi?
JIBU:
(Hukmu ya Qur-aan iliyomo katika) Simu za mkononi, si (sawa) kama Qur-aan yenyewe (Msahafu) bali hiyo ni dijitali; kwa hiyo anaruhusiwa kuibeba au kuishika.
[Sharh ‘Umdatil-Fiqh, kanda Namba 7, swali namba 24]
