Mahshiy Kusa -Mamumunya Yaliyojazwa - (Shaam)
Mahshi Kusa - Mamumunya Yaliyojazwa - (Shaam)
VIPIMO
Kusa ndogo ndogo - 1 Kilo
Nyama ya kusaga - ½ kilo
Tangawizi iliyosagwa -1 kijiko cha chai
Mchele wa Kimisri (Egyptian rice) -1 kikombe
Kitunguu maji (chopped au kilichosagwa) - 1
Garam masala ya unga - ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 1 kibati
kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 3 chembe
Mafuta ya zaytuni - 3 Vijiko vya supu
Pilipili manga ya unga -1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).
Baqduni (parsley) na kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo - ½ kikombe
Maji - 2 Vikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kaanga vitunguu katika kwa mafuta moto mdogo mdogo hadi vigeuke viwe laini au vibadilike rangi ya brauni iliyo khafifu.
- Tia nyama, thomu na tangawizi, garam masala, pilipili manga, chumvi na endelea kukaanga ipikike.
- Tia mchele na uchanganye vizuri.
- Zikwangue (toa nyama ya ndani) kusa ziwe na shimo, osha na weka tayari kwa kujazwa.
- Jaza na mchanganyiko huo wa nyama na mchele katika kusa.
- Panga vipande vya viazi chini katika sufuria na upange juu yake Kusa.
- Katika bakuli, changanya nyanya ya kopo na maji ya moto kidogo, thomu iliyosagwa, mafuta ya zaituni, pilipili manga, chumvi, chambua vidonge vya Maggi, tia baqdunis na kotmiri na uchanganye vizuri.
- Mimina sosi hiyo juu ya kusa, funika vizuri kwa kuwekea kitu kizito juu yake na pika moto wa kiasi kwa muda wa saa.
- Epua, funua itoke mvuke, pakua kusa katika sahani na pambia viazi juu yake, ikiwa tayari kuliwa.