Wali Wa Samaki Na Mboga
Wali Wa Samaki Na Mboga
VIPIMO VYA SAMAKI
Samaki wa sea bass vipande - 1 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau - 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Ndimu
Mafuta - 3 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
- Washa oven moto wa 400F.
- Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
- Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA
Gwaru (green beans) - 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Karoti - 4-5
Chumvi - Kiasi
Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga - 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni - Kiasi
Gwaru (green beans) - 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Karoti - 4-5
Chumvi - Kiasi
Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga - 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
- Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
- Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
- Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
- Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.