Wali Wa Kisomali Wa Kuku
Wali Wa Kisomali Wa Kuku
Vipimo
Mchele - 3 vikombe
Vitunguu (viliokatwa vidogo vidogo) - 2
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau - 1 kijiko cha supu
Mdalasini - 1 kijiti
Hiliki - 3 chembe
Pilipili manga nzima - chembe chache
Siagi - Vijiko 2 vya supu
Chumvi - kiasi
KUKU
Kuku kidari (Breast) kata vipande vipande - 2 LB
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo - kiasi
Bizari ya pilau (cummin au jiyrah) - 1 kijiko cha chai
Pilipili kubwa tamu la kijani - 1
Pilipili kubwa tamu nyekundu - 1
(zikate vipande vipande)
Karoti iliyokunwa - 1 – 2
Chumvi - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Wali:
- Roweka mchele kwa muda fulani kutegemea mchele
- Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vibadilike rangi kidogo.
- Tia thomu iliyosagwa, mdalasini, bizari ya pilau, hiliki, pilipili manga na chumvi, kaanga kidogo.
- Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji ya moto kiasi kutegemea na aina ya mchele kama kawaida ya kupika wali kama pilau.
- Tia sigai, funika upikike wali hadi uwive.
Kuku:
- Mchanganye kuku pamoja na thomu/tangawizi iliyosagwa, chumvi, pilipili mbichi.
- Katika karai tia mafuta yapate moto vizuri.
- Mtie kuku, bizari ya pilau (jiyrah) na ukaange, karibu na kuiva tia vitunguu.
- Tia mapilipili makubwa, kotmiri, na kaanga kwa dakika moja tu uzime moto na epua weka kando.
Kupakua:
Pakua wali katika sahani.
Pambia karoti iliyokunwa na ukipenda zabibu na wali uko tayari kuliwa