Keki Ya Jibini Ya Nanasi (Pineapple Cheese Cake)
Keki Ya Jibini Ya Nanasi (Pineapple Cheese Cake)
Vipimo
Malai ya Jibini (Cream Cheese) - 450g Pakiti 2
Sukari - 1/2 Kikombe
Mayai - 2
Unga wa ngano - 1 Kijiko cha chai
Mtindi (yogurt) - 1/2 Kikombe cha chai
Ukoko wa tayari (ready crust) - 2
Mananasi ya kopo - 1
Kastadi ya unga - 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni 350°F.
- Kwenye bakuli la mashine, changanya malai ya jibini, sukari, mtindi na unga upige hadi ichanganyikane vizuri.
- Kisha tia mayai na upige kidogo.
- Ikisha changanyika vizuri mimina juu ya ule ukoko (crust) na utandaze kila kipembe.
- Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 15, kisha weka moto wa 300°F na uchome kwa muda wa saa moja.
- Ikishaiva iache ipoe na huku uitayarishie sosi yake.
- Katika kisufuria, tia ile juisi ya mananasi utakayoitoa kwenye kopo, pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga hadi iwe nzito.
- Mimina juu ya Keki Ya Jibini na upange mananasi. Ukipenda weka cheri au jelly katikati ya duara ya mananasi.
- Iweke kwenye friji ipate baridi na itakuwa tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:
Unaweza ukagawanya vipimo mara mbili ukatoa keki moja.