Shaykh Fawzaan: Vipi Kumtolea Salaam Na Kumuombea Du’aa Maiti Kaburini?

 

Vipi Kumtolea Salaam Na Kumuombea Du’aa Maiti Kaburini?

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Vipi tutamtolea Salaam mtu aliekufa na kuzikwa?  Baadhi ya watu utamuona anasimama na kulielekea kaburi kisha anamuombea du’aa maiti, na mwingine anakaa chini akilielekea kaburi ananyanyua mikono yake na kuomba du’aa.  Ni ipi njia iliyo sahihi na iliyoruhusiwa ki-Shariy’ah  katika jambo hili?

 

 

JIBU:

 

 

Utamtolea Salaam maiti kama unavyomsalimia alie hai; utauelekea uso wake na utasema:

 

السلام عليك يا فلان ابن فلان ورحمة الله وبركاته

“Amani iwe juu yako ee fulani bin fulani, na Rahama za Allaah na Baraka zake.”

 

 

Kisha ukitaka kumuombea Du’aa, utalijaalia kaburi lake kati yako wewe na Qiblah -ukiwa unalielekea- utamuombea kwa Allaah Maghfirah (Amghufurie) na Rahmah (Allaah Amrehemu) na Ridhwaan (Allaah Amridhie) na wala hakuna ubaya wa kunyanyua mikono yako wakati wa kuomba du’aa.

 

 

[Fataawaa Shaykh Swaalih Bin-Fawzaan Al-Fawzaan: Mawqiful-Muslim minal-fitani   Ukurasa (36) ]

 

 

 

 

 

 

 

Share