Imaam Al-Bayhaqiy: Kuutukuza Mswahafu: Haijuzu Kuuwekea Kitu Juu Yake
Kuutukuza Mswahafu: Haijuzu Kuuwekea Kitu Juu Yake
Imaam Al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah)
Shaykh As-Sunnah An-Nabawiyyah Imaam Al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Haiwekwi juu ya Mswahafu kitabu kingine wala nguo wala kitu chochote ila isipokuwa ni Mswahafu mwingine juu yake.”
[Al-Bayhaqiy - Shu’ab Al-Iymaan (2/329)]
Faida:
Hiyo ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo kuhusu kuadhimisha Vitu Vitukufu Vyake, Alama Zake za Dini na kadhalika:
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ
Ndio hivyo iwe na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni khayr kwake mbele ya Rabb wake. [Al-Hajj: 30]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾
Ndivyo hivyo, na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 32]