Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mtu Aliyetubia Dhambi Asitaje Dhambi Zake Kwa Watu Bali Ajisitiri
Mtu Aliyetubia Dhambi Asitaje Dhambi Zake Kwa Watu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaan Ibn Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Haifai kwa mtu aliyetenda dhambi na akatubia kutokana na dhambi hiyo, kisha kumuambia mtu kuwa yeye alifanya dhambi, kwani kufanya hivyo ni kuikashifu stara ya Allaah (‘Azza wa Jalla) kwako.
[Fataawaa Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn (1/14)]
