Shaykh Fawzaan: Kushikamana Na Sunnah Si Jambo Sahali Kuna Mitihani Kadhaa
Kushikamana Na Sunnah Si Jambo Sahali Kuna Mithani Kadhaa
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)
Amesema Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)
"Kushikamana na Sunnah sio jambo sahali; kuna mitihani ndani yake, baadhi ya watu watakufedhehesha na watakuudhi na watakudharau na watasema: ‘Huyu ni mtu mutashaddidi, ametengana na watu’ au huenda wasitosheke na maneno na huenda wakakuua au wakakupiga au wakakufunga ikiwa unataka kuokoka na kunywa katika Al-Hawdhw hili. Subiri na ushikamane na Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hadi ukutane naye katika Al-Hawdhw (Hodhi)"
[Sharh Ad-Durrah Al-Mudhwiyyah uk 190]
Faida: Al-Hawdhw ni Hodhi la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali, na yenye harufu nzuri kuliko hal-miski. Urefu wake hodhi hilo ni mwendo wa mwezi mzima, na upana wake mwendo wa mwezi mzima.na vyombo vyake vinang'aa kama nyota za mbinguni. Watakaojaaliwa kunywa humo kinywaji chake ni wale Waumini watakaoshikamana na Sunnah.