081-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Mazungumzo Baada ya Ishaa ya Mwisho
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة الحديث بعد العشاء الآخرة
081-Mlango Wa Ukaraha wa Mazungumzo Baada ya Ishaa ya Mwisho
Hadiyth – 1
عن أبي بَرْزَةَ رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كان يكرهُ النَّومَ قَبْلَ العِشَاءِ والحَديثَ بَعْدَهَا . متفقٌ عليه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Barzah (Radhwiya Allaah 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya Ishaa na mazungumzo baada yake. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى العِشَاء في آخِرِ حَيَاتِهِ ، فَلَمَّا سَلَّمَ قال : (( أرأيْتَكُمْ لَيْلَتَكُمْ هذِه ؟ فَإنَّ عَلَى رَأسِ مِئَةِ سَنَةٍ لاَ يَبْقَى مِمَّنْ هُوَ علَى ظَهْرِ الأرْضِ اليَومَ أحَدٌ )) . متفق عليه .
Imepokewa kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliswalisha Ishaa katika mwisho wa maisha yake, pindi alipomaliza alisema: "Munajua kitu kuhusu usiku wenu huu? Hakika mwisho wa miaka mia kutoka sasa, hakuna mtu yeyote ambaye yuko katika ardhi atabaki hai wakati huo." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّهم انتظروا النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَجَاءهُمْ قَريباً مِنْ شَطْرِ اللَّيْلِ فَصَلَّى بِهِمْ - يَعْنِي : العِشَاءَ - ثمَّ خَطَبنا فقالَ : (( ألاَ إنَّ النَّاسَ قَدْ صَلُّوا ، ثُمَّ رَقَدُوا ، وَإنَّكُمْ لَنْ تَزَالُوا فِي صَلاَةٍ مَا انْتَظَرْتُمُ الصَّلاَةَ )) . رواه البخاري .
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) anasimulia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliakhirisha usiku mmoja Swalaah ya Ishaa mpaka nusu ya usiku. Baada ya Swalaah alitukabili na kusema: "Baadhi ya watu waliswali na kwenda kulala lakini waliosuburi (ili kuwahi Swalaah ya jamaa) walikuwa katika Swalaah kuanzia walipoanza kuingojea." [Al-Bukhaariy]