082-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Mke Kukataa Mwito wa Mumewe Anapomuita Kitandani na Hana Udhuru Wowote wa Kisheria
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم امتناع المرأة من فراش زوجها
إِذَا دعاها ولم يكن لَهَا عذر شرعي
082-Mlango Wa Uharamu wa Mke Kukataa Mwito wa Mumewe Anapomuita Kitandani na Hana Udhuru Wowote wa Kisheria
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأبَتْ ، فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا ، لَعَنَتْهَا المَلاَئِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ )) متفق عَلَيْهِ .
وفي رواية : (( حَتَّى تَرْجعَ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapomuita mume, mkewe kwenye firasha (kwa jimai) na asije, hivyo mume kulala akiwa na hasira, mke analaaniwa na Malaaikah mpaka kunapopambazuka." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah nyengine: "Mpaka atakaporudi (na kumtekelezea mumewe mahitaji yake)."