60-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

60:   Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini  

 

(08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja

 

Imepokelewa toka kwa Rifa’ah bin Raafi Az-Zuraqiy (Radhwiya Allaah ‘anhu):

 

قَالَ كُنَّا يَوْمًا نُصَلِّي وَرَاءَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرَّكْعَةِ قَالَ ‏"‏ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ ‏"‏‏.‏ قَالَ رَجُلٌ وَرَاءَهُ رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْدًا كَثِيرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيهِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ ‏"‏ مَنِ الْمُتَكَلِّمُ ‏"‏‏.‏ قَالَ أَنَا‏.‏ قَالَ ‏"‏ رَأَيْتُ بِضْعَةً وَثَلاَثِينَ مَلَكًا يَبْتَدِرُونَهَا، أَيُّهُمْ يَكْتُبُهَا أَوَّلُ ‏"‏‏

 

“Tulikuwa siku moja tunaswali nyuma ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na aliponyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu alisema:  Sami’a Allaah liman hamidah (Allaah Amemsikia aliyemhimidi).  Mtu mmoja nyuma yake akasema:  Rabbanaa walakal hamdu, hamdan kathiyran mubaarakan fiyh (Ee Mola wetu, ni Yako himdi, himdi nyingi njema iliyo na baraka ndani yake).  Alipomaliza swalah akauliza:  Nani aliyetamka?  Nikasema:  Ni mimi.  Akasema:  Nimewaona Malaika thelathini na kidogo hivi wakilishindania, nani awe wa mwanzo kuliandika kabla ya mwenziye”[Swahiyhul Bukhaariy (799)]

 

Hadiyth hii inatufunza fadhla kubwa ya kumhimidi Allaah na kumdhukuru, na pia uhalali kwa maamuma kusoma dhikri kwa sauti kidogo nyuma ya imamu bila kumbughudhi aliye karibu yake.

 

 

Share