Tahadhari Na Misemo Ya Istihzai, Masikhara, Ambayo Ni Kukufuru!: Kumlinganisha Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) Na Firawn Kwa Kusema: “Ukistaajabu Ya Muwsaa Utayaona Ya Firawn"

 

 

Tahadhari Na Misemo Ya Istihzai, Masikhara, Ambayo Ni Kukufuru!

 

 

Kumlinganisha Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) Na Firawn Kwa Kusema:

“Ukistaajabu Ya Muwsaa Utayaona Ya Firawn.”

 

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Haijuzu kamwe Manabii na Rusuli wa Allaah kulinganishwa na watu waovu! Na kufanya hivyo ni dhambi kubwa kwa sababu ni kumfanya Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) kana kwamba yeye alikuwa ana maovu ya kustaajabisha, ilhali Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewachagua Manabii na Rusuli Wake na Amewakatasa na maovu!  

 

Makosa haya yanaweza kumtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu kufanya istihzai (masikhara) katika yanayohusiana na Dini ya Allaah ni kukufuru!  Na dalili ni Aayah Alizoteremsha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuwahusu watu waliofanya istihzai (masikhara) katika Dini wakadai kuwa walikuwa wanaporoja tu na kufanya mzaha. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾

 

Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza. Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?

 

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ   

 

Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.

 

[Suwrah At-Tawbah (9:65-66)]

 

 

 

 

Share