Tambi Za Kukaanga Na Lozi
Tambi Za Kukaanga Na Lozi
Vipimo:
Tambi za kawaida - 1 paketi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Maji - 3 vikombe
Maziwa (carnation milk) - 1 kikombe
Sukari - 1 kikombe
Hiliki - 1/2 kijiko cha chai
Lozi - 1/2 kikombe
Zabibu - 1/2 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chambua lozi maganda uzikatekate (diced) uweke kando
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi hadi ziwe nyekundu.
- Tia maji, maziwa, sukari, hiliki, nusu ya lozi na zabibu.
- Acha zichemke hadi na kukauka zikiwa bado zina maji kidogo, ziepue.
- Paka siagi kidogo katika kikaangao (frying pan) iliyo na shimo kidogo (deep).
- Mimina tambi katika kikaango.
- Didimiza kwa mwiko kuzisawazisha zijifunge katika duara.
- Nyunyiza lozi na zabibu zilizobakia juu yake.
- Kata karatasi (kitchen paper) umbo la duara saizi kidogo kubwa kuliko ya kikaango. Irashie rashie (sprinkle) na maji kidogo iwe maji maji.
- Funika mkate kwa kitchen paper, rudisha katika moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 20, na kutambua kuwa mkate uko tayari ni maji yatakapokauka katika kitchen paper na ikawa kavu.
- Epua, toa kitchen paper, na upindue katika sahani, kisha katakata silesi au upendavyo.
Kidokezo:
Ikiwa huna maziwa ya carnation, tia maziwa ya kawaida vikombe 4 badala yake na badala ya maji.