Jina La Hudhayfah Ni La Kiume Au La Kike?

 

SWALI:

assalam aleykum napenda kuchukua nafasi hii kuuliza swali moja juu jina la

 HUDHAIFAH ni lakike au lakiume? 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 Hakika ni jina la Hudhayfah ni jina la mwanamume na miongoni mwa Maswahaba waliyoitwa jina hilo ni Hudhayfah bin Al-Yamaan, Abu Hudhayfah bin 'Utbah.

Shaka imekuja katika kudhani ni jina la kiume au la kike ni kutokana na linavyomalizikia jina lenyewe kwa taa marbuutwah (taa iliyofungwa inayodhihirisha jinsia ya kike) ambayo kwa kiswahili huwa inaishia na herufi ya 'h'. Na hii ni kawaida ilivyo  katika sarufi (grammar) ya Kiarabu. 

Mifano ya majina kama hayo ni; Hamzah, 'Ikrimah, Usaamah, Qataadah, 'Attwiyyah n.k.

Na majina ya kike ni vizuri  kuchagua majina ya wanawake wema na watukufu kama wake zao Mitume, Maswahaabiyaat na wengineo waliotajwa katika historia yetu. 

Kwa maelezo zaidi kuhusu majina ya watoto soma mada katika viungo vifuatavyo:

 

 

Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto

 

 Majina Ya Watoto Na Maana Yake

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share