Kuwaosha Watoto Wachanga Kwa Majimbo Kwa Ajili Ya Siha Na Kuwakinga Maovu Inafaa?
SWALI:
Shukran kwa kutujibia masuali yetu na Inshallah Allah atakulipeni mema na muzidi kutusaidia ndugu zenu katika Imani.
Suali langu ni, katika jamii zetu hususan huku Tanzania tangu miaka ya nyuma, wazee wetu wakijifungua huwa watoto wao wanawakosha majimbo ili mtoto akue na achangamke uzuri na aingie mwili akazane. Pia
Je hii ni sahihi? Na
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji swali kuhusu suala la ‘majimbo’. Kulingana na muulizaji inaonyesha
Kwa hivyo, suala ambalo tutaliangazia ni kuhusu njia gani tunafaa tuwakinge watoto pamoja na kujikinga sisi wenyewe. Kinga ni zile tulizopatiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kinyume na hivyo hatutakuwa ni wenye kufaulu wala kupata kinga ya uhakika na mara nyingi tutakuwa tunanyonywa. Kwa kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) peke Yake ndio tunapata kinga na hakuna madhara yanayoweza kutufika.
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anatueleza:
“Sema: Halitusibu ila Alilotuandikia Allaah. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Allaah tu!” (9: 51).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuusia Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) na hivyo kutuusia sisi:
“Jua kwamba hakika lau watu wakusanyike ili wakunufaishe wewe kwa jambo lolote, hawawezi kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakikusanyika ili kukudhuru kwa jambo lolote, hawawezi kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah” (at-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh).
Kinga anazopata mtoto zinaanza kuanzia wakati baba anapomchagulia mama. Dini ni kinga kubwa kwa wanandoa na vizazi vyao vitakavyopatikana. Kinga yenyewe inaanza pale mwanamme kabla ya kuposa anaposimama kuswali rakaa mbili ili kumtaka ushauri Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na mwanamke naye afanye vivyo hivyo. Hii ni Swalah ya Istikhaarah ambayo Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anatuelezea kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwafundisha Swalah hiyo
Baada ya posa na wanandoa kuungana katika Nikaah, ni Sunnah kwa mume kusema anapoingia kwa mkewe siku ya mwanzo du’aa ifuatayo:
“Allahumma inniy as-aluka khayrahaa wa khayra maa jabaltahaa ‘alayhi wa a’udhu bika min sharrihaa wa sharri maa jabaltahaa ‘alayhi – Ee Allaah! Nakuomba kheri yake na kheri aliyokuja nayo na uniepushe na shari yake na shari aliyokuja nayo” (Abu Daawuud na Ibn Maajah).
Usiku huo wa mwanzo baina ya mume na mke si usiku wa starehe tu bali ni lazima watekeleze amri za Dini, na katika hayo ni Swalah. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Atakapooa mmoja wenu na ikawa ni siku ya mjengo na aswali rakaa mbili na amuamuru mkewe aswali nyuma yake kwani Allaah Atajaalia katika nyumba hiyo kheri” (al-Bazzaar).
Kinga ya mtoto pia inapatikana kwa mume kuomba du’aa aliyotufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati mtu anajamiiana na mkewe kwa kusema:
“Bismillaahi Allaahumma jannibnash Shaytwaan wa jannibish Shaytwaana maa razaqtanaa – Kwa jina la Allaah, Ee Allaah! Tuepushe na Shetani na Umuepushe kwa kile utakachoturuzuku”. Akizaliwa mtoto Shetani hataweza kumdhuru (al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas [Radhiya Allaahu ‘anhuma]).
Mtoto pia anakingwa hasa na magonjwa kwa kupatiwa lishe bora na katika siku za mwanzo kunyonyeshwa. Maziwa ya mama hasa kwa wiki za mwanzo yana kinga kubwa
“Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada” (2: 233).
Mama kupata lishe bora ni njia moja ya kuwakinga watoto kutokana na maradhi. Na pindi mtoto anapokuwa mgonjwa basi mtoto anafaa kupelekwa na wazazi wake hospitali ili atibiwe.
“Hakika kila ugonjwa una dawa, ikisibu dawa ugonjwa anapona kwa idhini ya Allaah Aliyetukuka” (Muslim na Ahmad).
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) ndiye Mwenye kuponyesha
“Na ninapougua ni Yeye ndiye Anayeniponesha” (26: 80).
Ama kinga nyingine, ni kusoma Aayah kumi za Suratul-Baqarah ambazo zinaleta natija kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) kuiepusha nyumba hiyo na kuingiliwa na mashetani. Ayah zenyewe ni
“Ikifika jioni wazuilieni watoto wenu kutoka toka kwani mashetani wanatawanyika nyakati hizo … fungeni milango na mtajeni Allaah mnapoifunga kwani Shetani hafungui mlango uliofungwa” (al-Bukhaariy na Muslim).
Kinga nyingine kubwa ya watoto ni vile alivyokuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwafanyia wajukuu zake, al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwa kuwasomea: “U‘idhukumaa bikalimatiLlaahi at-Tammaati min kulli Shaytwaaniw wa haammah wa min kulli ‘aynil laamah – Nawakinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia, Awakinge kutokana na kila Shetani, na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru” (al-Bukhaariy).
Ama kinga hiyo wanayofanyiwa watoto wa sehemu uliyopo haina faida yoyote na haijapokewa katika machimbuko ya Kiislamu ya kisheria. Inawezekana kuwa hayo ‘majimbo’ kama mnavyoita yanawafanya kweli watoto wawe wachangamfu lakini huo ni mtihani kwani Shetani huwa akiwapambia wanaadamu mambo
Tunakuombea kila la kheri katika kuondosha munkari
Na Allaah Anajua zaidi.