Jina La Nasra Linafaa Kutumika? Kwani Ni Jina La Sanamu Wa Zama Za Nuuh
SW
Assalaykum warahmatullahi wabarakatuh.
Mtume wetu Muhammad (SAW) ametuusia kupeana majina mazuri na tusiitane majina mabaya. Swali liko hivi jina la Nasra ni zuri lakini ukiaangalia katika
وَقَالُوا لاَ تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلاَ تَذَرُنَّ وَدّا ً وَلاَ سُوَاعا ً وَلاَ يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرا
23. Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.
Sasa jee inafaa kumwita mtoto jina la Nasra au haina neno naomba nifafanuliwe zaidi. wabilahi tawfiq.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuitwa mtoto msichana kwa jina la Nasra. Tunapenda awali ya yote mwanzo kueleza yafuatayo, ifahamike kuwa majina haya Wadd, Suwaa', Yaghuuth, Ya'uuq na Nasra yalikuwa ni majina ya watu wema waliokuwa kabla ya Nabii Nuuh (‘Alayhis Salaam). Hawa Waumini walikuwa msitari wa mbele katika kufanya mema na kusaidia wenziwao pamoja na kufanya Da'wah. Walipokufa Ibliys alikuja kwa jamii hiyo na kuwachezea mpaka wakaanza kuwaabudu.
Kwa ajili ya 'Ibadah hiyo ambao walifanyiwa hao, ndio Uislamu ukawa ni wenye kufunga njia ya kuyaendea maovu kwani mtoto akiitwa jina
Baada ya kusema hayo inaonekana kuhusu jina
نَسْرا (Nasra)
نَصْرة (Naswrah)
Tukitizama majina hayo mawili juu tutaona tofauti ya wazi kabisa. Jina linalotumika katika majina wanayoitwa au kupewa mabint lina Swaad, Naswrah (la kike) na Naswr au Naaswir (la kiume), na sio Nasr
Tuna imani kuwa ufafanuzi huo utakuwa umesaidia kuondoa utata huo.
Na Allaah Anajua zaidi