Avunje Ndoa kwa sababu Walizini Kabla ya Ndoa?
SWALI:
Sheikh suala hili linanitatisha
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa muulizaji swali hili. Na inaonyesha kuwa mas-ala haya ya uasherati au mafungamano ya kimwili baina ya mume na mke yamekithiri. Inatakiwa tuwe ni wenye kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) popote tulipo na kila wakati. Na
Mwanzo inatakiwa tufahamu kuwa zinaa ni kitendo kibaya
Ni wazi kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Husamehe madhambi yote ikiwemo dhambi la uzinzi
“Sema: Enyi waja Wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na rehema ya Allaah; bila shaka Allaah Husamehe dhambi zote; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu” (39: 53).
Na hasa kuhusu kusamehewa dhambi la zinaa, anasema Aliyetukuka:
“Na wale wasiomwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara. Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyaama, na atadumu humo kwa kufedheheka. Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu
Kisha ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi katika mas-ala
Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika
Na kuhusu mas-ala ya kusamehewa kwa dhambi
“Mche Allaah popote ulipo. Na ufuatilize jambo baya kwa jema, litalifuta (
Kuhusu mas-ala haya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Mwanamume mzinifu hatamwoa ila mwanamke mzinifu au mwanamke mushrik, na hamna atakayemwoa mwanamke mzinifu isipokuwa mwanamume mzinifu au mushrik; na ndoa
Ikiwa watu hao wawili wamefanya zinaa wanaweza kuoana kisheria baada ya kutenganishwa kwa muda. Muda huu ni wa kuhakikisha kuwa yule mwanamke hana mimba yoyote na kwa sababu binti hakuwa na mimba basi hakuna tatizo la wao kuoana. Muda unaweza kuanzia miezi mitatu au kutegemea uamuzi wa Qaadhi ikiwa katika sehemu hiyo yupo mmoja.
Kuhusu Aayah hizi anasema Ibn Kathiyr: “Amesema Imaam Ahmad kuwa haifai ndoa baina ya wazinifu mpaka watubu, akitubu inasihi Nikaah. Na hivyo ndivyo alivyosema Imaam Abu Muhammad bin Abi Haatim ambaye amemnukuu Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa alikuja mtu ambaye amezini akamuuliza
Hakika ni kuwa wametofautiana wanazuoni wa zamani katika jambo hili katika makundi mawili:
a) Kuharamishwa ndoa, nayo ni rai ya ‘Aliy, al-Baraa’, ‘Aaishah na Ibn Mas‘uud (Radhiya Allaahu ‘anhum).
b) Kujuzu ndoa na aliyezini, nayo ni rai ya Abu Bakr, ‘Umar, Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhum) na ni madhehebu ya Jamhuur na huo ndio msimamo wa Mafakihi wanne na Maimamu waliojitahidi.
Dalili za Rai ya Kwanza
Wametoa dalili wanaoharamisha kwa dhahiri ya ayah nayo ni kauli ya Aliyetukuka:
“Mwanamume mzinifu hatamwoa ila mwanamke mzinifu au mwanamke mushrik” (24: 3).
Wakasema: Dhahiri ya Aayah hii ni habari na uhakika wake ni kukataza na kuharamisha kwa dalili nyengine katika Aayah hiyo:
“Na ndoa
Na amesema ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu): Anapozini mtu yeyote anatenganishwa baina yake na mkewe, na hivyo hivyo akizini mke.
Na wametoa dalili kwa yaliyotokea kwa Marthad bin Abi Marthad (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa Swahaba, naye alizini na ‘Inaaq, mwanamke malaya Makkah wakati wa ujahiliya. Alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kumuomba ruhusa amuoe. Alimuomba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) mara mbili bila kujibiwa. Alipomuomba mara ya tatu, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alimsomea Aayah hii na akamwambia asimuoe (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).
Na zipo Hadiyth nyengine kutoka kwa Ibn ‘Umar na ‘Ammaar (Radhiya Allaahu ‘anhum) zinazoelezea jambo
Dalili za Rai ya Pili (Rai ya Jamhuur)
Wametoa dalili zao kwa kuruhusiwa ndoa
(i) Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu mtu aliyezini na mwanamke na akataka kumuoa, akasema: “Mwanzo ni uchafu na mwisho ndoa, na haramu haifanyi halali kuwa haramu” (atw-Twabaraaniy na ad-Daaraqutwniy).
(ii) Iliyopokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa: “Alipokuwa Abu Bakr yuko Msikitini mara akaja mtu ambaye alikuwa anataka kumwambia kitu lakini hakuweza kueleza kwa ufasaha. Abu Bakr alimwomba ‘Umar amchukue yule mtu kando ili amdadisi kuwa anataka kusema nini. Alipomwuliza, alimwambia kuwa kuna mgeni aliyemtembea naye amezini na binti yake. Hapo ‘Umar alimpiga kwenye kifua chake na kumwambia: ‘Ole wako, kwa nini usingesitiri aibu ya binti yako?’ Abu Bakr aliamuru wote wawili wapatiwe adhabu, kisha akawaoza na kuhamishwa mbali na mji kwa mwaka mmoja” (Qaadhi Abu Bakr Ibn al-‘Arabiy, Ahkaamul Qur-aan, Mj. 3, uk. 1319).
(iii) Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliulizwa kuhusu mas-ala hayo, akasema: “Mwanzo ni uchafu, na mwisho ni ndoa. Mfano wa
iv) Wameawili Aayah hii tukufu: “Mwanamume mzinifu hatamwoa ila mwanamke mzinifu au mwanamke mushrik” (24: 3). Hii imechukuliwa kwa ujumla na wingi wake, na maana yake ni kuwa fasiki (asi) mwovu ambaye ni mzinifu hatamani kuoa Muumini mwanamke mwema, hakika ni kuwa yeye ana hamu ya kuoa aliye asi mwovu mfano wake au mshirikina. Na mwanamke asi mbaya hana hamu ya kuolewa na Muumini mwema miongoni mwa wanaume, kwani hakika yake ni kuwa yeye ataka jinsi ya mfano wake wa asi na mushirikina.
(v) Na wamesema baadhi ye wengine: Aayah hii hukumu yake imetenguliwa na Aayah nyengine ya Suratun Nuur: 32 (Tafsiyr Aayaatul Ahkaam minal Qur-aan, Mj. 2, uk. 36 – 37).
Na Dkt. ‘Aliy ‘Abdul-Haliym Mahmuud katika kitabu chake at-Tarbiyyatul Islaamiyyah Fiy
‘Haoi mzinifu aliyepigwa mijeledi isipokuwa mfano wake’ (Abu Daawuud). Na wanazuoni wengine wanasema Aayah hii ilikuwa ni hasa kwa Marthad (Radhiya Allaahu ‘anhuma) na kahaba aliyeitwa ‘Inaaq. Na wengine wanasema yeyote mwenye kuzini na mwanamke anafaa amuoe na asiolewe na mwengine yeyote, nayo ni kauli ya Ibn ‘Umar, Saalim, Jaabir ibn Zayd, ‘Atwaa’, Twaawuus, Maalik ibn Anas na Abu Hanifah”.
Kwa muhtasari ni kuwa wazinifu wakitubia na kujirekebisha basi wanaweza kuoana. Ondoa wasiwasi wako kuhusu ndoa yako kwani wasiwasi unaletwa na shetani naye kwetu ni adui wa wazi kabisa isipokuwa uwe unataka kumuacha kwa nafsi yako mwenyewe.
Na Allaah Anajua zaidi