Mtoto Asiyenyonyeshwa Na Mama Yake Inapasa Alipwe?
SW
Jee kuna aya inayoelezea kumlipa mtoto usipomnyonyesha katika quraan naomba ufafanuzi?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumlipa mtoto ukitomnyonyesha.
“Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na
Hata hivyo kwa mama kutomnyonyesha mtoto wake bila udhuru wowote si jambo zuri kwani maziwa ya mama yana faida kubwa kwa mtoto. Maslahi ya mtoto ni lazima yatizamwe.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Je Kuna Malipo Kama Hukumnyonyesha Mtoto?
Kumnyonyesha Mtoto Ambaye Sio Wa Kumzaa
Na Allaah Anajua zaidi