Bajia Za Dengu Na Viazi
Bajia Za Dengu Na Viazi
Vipimo
Unga wa dengu - 3 vikombe vikubwa
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Mbatata (kiazi) - 2
Maji baridi - 1 glass
Baking powder - 1 cha chai
Kotmiri iliyokatwakatwa - 4 -5 Miche
Kitunguu maji -1
Kitunguu saumu (thomu) ilosagwa au ya unga - 1 kijiko cha chai
Mafuta - 500 ml
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi katakata vipande vidogodogo.
- Menya kitunguu katakataka slesi ndogo ndogo kiasi
- Katakata (chop) kotmiri
- Tia unga wa dengu katika bakuli, changanya pamoja na chumvi na baking powder.
- Mimina vitu vyote katika bakuli pamoja na kitunguu thomu ulosaga.
- Tia maji ukitumia uma au mchapo wa mkono (usotumia umeme) kuvuruga mchanganyo.
- Ukisha kuwa laini bila mavimbo, hakikisha si mzito na si uji sana (mwembamba).
- Uwache kwa muda wa robo saa (dakika 15) paka 20.
- Weka karai jikoni au sufuria nzito ndogo, tia mafuta na acha yapate moto sawasawa.
- Tumia kijiko cha supu kuteka unga kutia kwenye mafuta , unapotia hakikisha kipimo chako chote kimelenga mahala au sehemu moja bila ya kutapakaza ili uweze kupata kidonge .
- Utaenedelea hivi kwa kujaza karai nafasi yote zikigeuka rangi ya kuiva, unazigeuza upande wa pili paka umalize zikiwiva kwa rangi nzuri.
- Tumia sahani ukiwa umetandaza karatasi za jikoni kuweza kuchuja mafuta baada ya kuchoma. Kisha badilisha kwenye sahani au bakuli nyengine, tayari kuliwa
Kidokezo:
Huliwa kwa chatini ya aina yoyote.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)