Vibibi Vya Tui
Vibibi Vya Tui
Vipimo
Mchele - 2 Vikombe
Tui la nazi zito - 2 Vikombe
Hamira - 1 Kijiko Cha chai
Unga wa ngano - 2 vijiko vya supu
Iliki - kiasi upendavyo
Sukari - kiasi upendavyo
Yai - 1
Vipimo Vya Tui La Kupaka
Tui la nazi - 2 Vikombe
Iliki ya unga - Kiasi upendacho
Sukari - Kiasi upendacho
Unga wa ngano - 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo.
- Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito.
- Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
- Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
- Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya.
- Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
- Ukishafura , weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo)
- Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote.
- Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au samli kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko ukitumia upawa na ufunike.
- Kibibi kikianza kuiva na kushikana upande mmoja , kigeuze upande wa pili mpaka kigeuke rangi na kuiva.
- Panga kwenye sahani iliyopakwa tui.
- Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; kila ukiepua kibibi, panga juu ya mwenzake kama ilivyo kwenye picha na upake tui juu yake.